Wako wapi walioimba "We are the world" mwaka 1985?

Umemsahau marehemu RAY CHARLES huyu Mzee alikuwa mtata Sana kwenye maisha yake alafu alikuwa kipofu toka ana miaka 7 na alishawahi kutumia madawa ya kulevya Kwa kipindi kirefu..
Kuna movie moja inaitwa Ray imechezwa na Jamie fox inaelezea maisha ya ray Charles
hii ndio shida ya kutokusoma mpaka mwisho shida ni nini mkuu au kuna mashindano ya kutoa maoni
 
Duu aisee mbona hakuna Baya nimesema au kuna neno lolote nimekosoa? Mimi nimeongezea nyama Tu pia Mimi nimesifia Tu na hata mtoa mada anajua..

Yote ambayo mtoa mada amepost ni sahihi ndiyo maana Mimi nimejazia nyama Tu Kwa MTU mmoja Ray Charles ingawa ametajwa na mtoa mada
 
Mara ya kwanza naiona video nikajiuliza huyu ni nani mbona kama nimempenda ghafla,doh kumbe mimi ndio mgeni duniani.
Aina ya wanawake wa Diana Ross huwa wako wachache halafu ni kama ka mbegu flani kapo hivyo kuanzia nywele macho midomo na umbo lao huwa wako hivyo
Kuna msichana nilikuwa nae hakujua nimempenda sababu wamefanana sana na Diana
 
Michael alimpenda sana diana sema tatizo umri alikua mkubwa kuliko MJ,,,ana mtoto wake wakike hazeeki ana miaka 51
IMG_5059.jpg
 
Katika kipindi cha miaka ya 80 na miaka ya 90, ngoma za dance hall, Rock na mitindo mbali mbali ndiyo ilikuwa inabamba sana, sio sasa kama ilivyo amapiano, Bongo flavor, hip hop na afro beats.

Basi mwaka 1985 wasanii waliokuwa wanatamba miaka hiyo Michael Jackson na Lionel Richie wakaamua kutunga wimbo kwa ajili ya kusaidia Afrika na dunia kiujumla, nakumbuka kipindi hiki kulikuwa na njaa Afrika kama ile njaa ya Ethiopia ya mwaka 1984-85.

Enewei nisiwachoshe sana, nataka kuwakumbusha wasanii walioshiriki katika ngoma hii kwa sasa wapo wapi..

1. Lionel Richie
Kwa sasa bado yupo hai ana miaka 74, bado anafanya muziki, na ana tamasha la nchi 18, mwaka 2023-24.

2. Stevie Wonder
Bado yupo ngangali na muziki akifanya show mbali mbali akiwa na umri wa miaka 73, ikumbukwe Stevie ni mlemavu wa macho (kipofu).

3. Paul Simon
Ana miaka 82 hivi sasa, na anatarijiwa mwaka huu kutoa album yake ya 7 psalms, lakini tangu mwaka 2018, ameacha kusafiri Katika matamasha ya muziki.

4. Kenny Rodgers
Mzee wangu wa ngoma za country, nazipenda sana ngoma zake kama gambler na Lady, huyu kwa sasa ni marehemu alifariki mwaka 2020 mwezi Machi akiwa na miaka 81

5. James Ingram
Kaka kutokea Ohio, huyu pia alitangulia mbele za haki mnamo mwaka 2019 mapema mwezi wa kwanza akiwa na umri wa miaka 66.

6. Tina Turner
Akina mama zetu na baba zetu walibahatika kumuona akiwa kijana bi Anna Mae Bullock maarufu kama Tina Turner. Huyu kafariki mwaka huu machi 2023 akiwa na miaka 83, na kuzikwa kwao Switzerland.

7. Billy Joel
Miaka yake kwa sasa ni 74 bado yupo mitaa ya New York, bado anafanya muziki na pia aliwahi kujihusisha na siasa mwaka 2016.

8. Michael Jackson
'King of pop' 2009 mwezi June, ndio ulikuwa mwisho wa kumuona mfalme huyu wa jukwaani, alifariki akiwa na umri wa miaka 50.

Naomba niishie hapa, muda mwingine nitamalizia list yangu, maana hapa bado Roy Charles, Bruce Springsteenn. N.k

By Meshack Chavala
 
Attachments

  • VID-20210612-WA0251.mp4
    13.7 MB

Chris Hayes, Latoya Jackson (DADAKE MICHAEL JACKSON),Bill GIBSON NA wengine wengi HATA BONO wa U2 aliimba
 
Back
Top Bottom