Wako wapi watanzania waliosoma shule za vipaji maalumu.

Wako wapi watanzania waliosoma shule za vipaji maalumu.

Mzee wa fund

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Posts
514
Reaction score
89
Salamu wana JF. mimi nauliza hivi wale waliosoma zile shule za vipaji maalumu. wamelitendea nini taifa la Tanzania? maana walifundiswa na walimu wazuri, mazingira mazuri yaani maktaba, maabara, nk.

je baada ya muda wote huu kupita kama hawaja litendea chochote cha maana taifa letu, je kuna haja ya shule hizo kuitwa za vipaji maalumu.? nawasilisha.
 
Go figure!

Vipaji maalumu kwa viwango vya kibongo bongo si mali kitu mbele ya viwango vya wengine!

Bongo ukiwa mjanja mjanja uibe pepa upasue vi- A vyako kadhaa utaitwa una kipaji maalumu.
 
Hao vipaji maalum wa zamani si ndio hawa wanatusumbua leo na akaunti za EPA, ESCROW na marichmond, big results now na utumbo mwingine mwingi.
 
Nipo hapa mkuu

Kwa mazingira yale magumu,ukosefu wa walimu,vitabu,chakula kibaya na matatizo mengine,mimi na wenzangu tumemanage kusoma hadi elimu ya juu

Huku tumekutana na wenzetu waliosoma private schools ambao hawajatumia nguvu nyingi sana kufika hapa

“Uspesho“ wetu unakuja tu kwa sababu,kwa mazingira yale yale,tumeweza kufika elimu ya juu,kwa wingi,kwa michepuo ambao fani zake zinaongoza kwa upungufu wa wataalamu.

Hilo tu
 
Back
Top Bottom