Wakoloni walitutawala kwa kutumia akili zao na nguvu zetu, jambo ambalo limetushinda ni kutumia nguvu na akili zetu

Wakoloni walitutawala kwa kutumia akili zao na nguvu zetu, jambo ambalo limetushinda ni kutumia nguvu na akili zetu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wajerumani walianzisha miradi mikubwa mfano mashamba ya mkonge na viwanda vya katani pia ukuleles bandarini kwa kutumia pesa ya serikali.

Walianzisha kodi ya kichwa, hivyo kila raia mwenye umri wa miaka 18 -50 ilimpasa kufanya kazi ili alipe kodi.

Waliweka bidhaa madukani wakiwa na uhakika wa wateja kwani walijua wanalipa mishahara.

Kwa mipango endelevu wangeweza kusomesha nyumba za udongo na nyasi kwa kumkopesha kila mfanyakazi vidaka vya ujenzi na kumkata kwenye malipo yake.

Kikubwa na mzunguko wa pesa na mipango madhubuti maendeleo ya watu yanakuja bila kupenda.

Mkandarasi atatengeneza barabara, atajenga shule, atajenga soko. Kukiwa na barabara nzuri kuna watakaowekeza kwenye mabasi na watu watawahi makazini na mashuleni.

Raia wengi wakikosa ajira ni mzunguko wa umasikini.
 
Angalau leo umekuja na mada fikirishi. Inafanya watu wajue adui wa maendeleo yao ni nani.
 
Asante kwa bandiko,
Mstari wa mwisho ni mstari bora. Raia wakikosa namna ya kupata pesa, watashindwa kununua bidhaa na kugharamia huduma (umasikini) hivyo wauzaji wa bidhaa na huduma watakosa wateja ina maana kuwa biashara zitashindwa kuendelea (zitakufa), hii ni ishara kuwa hao wauza bidhaa na huduma watashindwa ku 'sustain' kwenye maisha yao (umasikini)- hapo ndio unapotengeneza chain of poverty (vicious cycle).

Jambo la msingi ni kukata hiyo chain isiendelee kuzunguka hizo wheels.
 
Serikali ikifanya kama Wakoloni mtalia udikteta, wakati wa Ukoloni vijana walikuwa wanakimbia vijiji vyao kutafuta hela ya kulipia kodi ya kichwa, leo hii hata nidhamu ndogo tu ya bar kufungwa na kufunguliwa jioni baada ya kazi watu wanalia udikteta wakati huo ulikuwa ni utaratibu wa Mkoloni, haujaanzishwa na Serikali yetu, tuliurithi.
 
Back
Top Bottom