Tuendelee kuchukua tahadhari zifuatazo:
1. Epuka mikusanyiko isiyo ya lazima (kaa umbali wa mita 2 kati yako na mtu mwingine).
2. Usipande gari lililojaza sana. Hakikisha unanawa kabla na baada ya safari. Kama safari sio ya lazima usiende.
3. Epuka kugusa uso, macho na pua kwa mikono isiyo safi.
4. Safisha simu yako mara kwa mara kwa maji kidogo na sabuni. Kipindi hiki, tuepuke kushikiana au kupeana simu.
5. Safisha vitasa, meza na vitu vyovyote vinavyotumika na watu wengi.
6. Nawa kwa maji safi tiririka mara kwa mara au tumia sanitizer pale ambako hakuna maji na sabuni. Msinawe maji ya kwenye chombo kimoja. Tumia maji tiririka. NAWA. NAWA. NAWA
7. Ukiwa na homa, mafua, kukohoa, koo kuwasha, maumivu ya viungo au kushindwa kupumua, jitenge ili kama ni ugonjwa wa Corona usiambukize wengine.
Toa taarifa na wataalamu wa afya watakuja kwako.
JIKINGE NA UWAKINGE WENGINE
Sent using
Jamii Forums mobile app