Wakongwe: Uliangalia wapi Fainali ya Kombe la Dunia 1994 kati ya Brazil VS Italia

ulimwengu usio na stress
Ulimwengu usio na stress na usio na hizi raha za dunia. Ukaamua kuja kupata raha na stress, huwa haziachani, endless circle.
Jambo la muhimu wewe zingatia raha, stress zipe ''airtime'' ndogo na ukubali kuwa ni sehemu ya maisha.
Na zile stress za kujitakia, hizo ziepuka pambana na zile za lazima tu ili upime ''strain power'' yako.
 
Magomeni kwa marehemu sheikh Yahaya
 
Miaka hiyo Tyson akiwa kwenye ubora wake mnakesha kusubiria pambano ukifika muda anamaliza ngoma ndani ya dakika tatu.

Waliolala wakiamka wanakuta jamaa kashamaliza.
ITV mwaka huo walituuza akina Mikidadi Mahmoud tunasubiria kumbe wenye madishi wanakula sisi tunangoja recorded....
 
Nimekuelewa mkubwaπŸ™
 
Niliangalia kwenye Kibanda-Umiza kwa Binamu yangu Deo Matengelele Visiga Kibaha. Kulikuwa na Mzee anakuja na tv na antena yake na kuonyesha mpira pale kupitia ITV.

Mashindano yale kiujumla yalikuwa bora hata kwa Cameroon ya mkongwe wa miaka 42 Roger Milla. Kulikuwa na bingwa wa kufunga magoli ya kichwa...mtu mweusi mmoja wa Sweden akiitwa Darlin.

Vya kale ni dhahabu kwakweli...
 
Yeah Martin Dahlin pande la mtu hivi.
 
niliangalia kwa jirani kituo itv, nlikuwa form 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…