Wakongwe: Uliangalia wapi Fainali ya Kombe la Dunia 1994 kati ya Brazil VS Italia

Mwamba kweli kweli Dan Martin Nataniel Dahlin huyu aliiwezesha Sweden kushika nafasi ya tatu kwenye World Cup ya 1994.

Alikuwa fundi kweli kweli.
 
Umenikumbusha. ITV zamani walikuwa wanaonyesha ligi ya Uingereza. Bure kabisa. Enzi Arsenal ikiwa na wachezaji kama kina Overmass, Tony Adams, etc...
Hata NBA pia
Ukitaka kuona marudio ublnasubiri tamasha la michezo j2 mchana
 
Hata NBA pia
Ukitaka kuona marudio ublnasubiri tamasha la michezo j2 mchana
Game za NBA zilikuwa zinaonyeshwa mchana, miaka ile Chicago Bulls na Milwaukee wapo moto sana na wale wengine Clippers.

Maisha yalikuwa tofauti sana.
 
Yeah...Tmk, Tandika, Chang'ombe, Kurasini na Aziz yote mpk Uwanja wa Sifa wote 77 Rongai Bar na zingine. Kumbuka mwaka huo ITV ndo akianza na hiyo ilikuwa moja ya promo zake.
Na bands la ujeruman
 
nilikuwa mpakani, tv inayo kamata ilikuwa tv rwanda na burundi hizi itv, channel 10 na nyingine za kibongo nimekuja zifahamu baada ya kuhama mpakani
ukamshuhudia Zidane LIVE bila chenga. hapo mimi ndio kwanza hata Uso sijui kunawa
 
Kombe LA KWANZA kabisa LA Dunia KUWAHI KURUSHWA na local TV channel ITV. KABLA ya HAPO ni WATU WA Masaki tu waliokuwa wnanagalia Kombe LA dunia KUPITIA Satellite dishes
Nilikuwa Manzese Tip Top
 
Sisi tuliletewa recorded mwaka 1997 huko Serengeti nikiwa darasa la saba,nakumbuka waliweka video kwenye stoo ya Kijiji [emoji1787][emoji1787]
 
Zamani mpira ulikuwa unachezwa haswa, yaani ilikuwa ni full maufundi, full burudani na wachezaji wazuri walikuwepo wengi sana ila mashabiki wengi tulikuwa hatuna access ya kupata burudani hiyo, wengi tulifuatilia mechi kupitia redio tu.

Miaka hii ambayo ndio Kuna access kubwa ya kuona mechi yoyote unayoitaka, mpira mzuri mzuri nao umekuwa adimu, timu nyingi zinacheza utopolo mtupu na wachezaji mafundi wenye vipaji asilia nao wameadimika.... !!

Binafsi Huwa nina enjoy sana, kuangalia mechi za zamani hasa za world cup kuanzia 1980s mpaka 2002 hapo. Hizi mechi ndio Huwa zinakula bando langu nikiingia YouTube.
 
ukamshuhudia Zidane LIVE bila chenga. hapo mimi ndio kwanza hata Uso sijui kunawa
Ufaransa haikuwepo kwenye World Cup ya 1994; kwenye mechi za kufuza kwa maajabu akachapwa na Bulgaria na Israel.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…