Wakongwe wa soka mnakumbuka hii njumu enzi hizo

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Nakumbuka ka- harufu kake ikiwa MPYA imetoka dukani
🤣😅
.
Wakuu Hivi Viatu Vilikuwa vinaitwa Abeid Mziba

Màana Yeye ndie mchazaji pekee alikuwa anatumia viatu hivi wakati huo ligi Daraja la kwanza kabla premier league
Ndio vikabatizwa jina lake...

 
Mohamed Husen " mumachinga" anisamehe . Niliwahi kumtandika kwa ndaruga hii 1995 mechi ya ligi kuu daraja la kwanza enzi hizo nikiwa no.4 pale msimbazi
 
aisee umenikumbusha mbalimbali sana! ilikuwa ikipauka navunja betri napaka kaa lake ili iwe nyeusi ivutie..
 
Mimi nilikua nacho chenye rangi nyeusi na njano! Kiliandikwa Roger Milla.

Hatari sana enzi hizo. Ishu ukikifua mara mbili tu!
 
Sema yale yalikuwa yanachanika hovyo Sana hasa ukiwa mpigaji wa Mashuti au beki ...
 
Aiseee wakati nipo beki kitasa nilitumia na nilikitendea haki...kilikuwa chekundu na njano.....COSOVO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…