Wakristo mmejipangaje kusimama na watumishi wenu?

Wakristo mmejipangaje kusimama na watumishi wenu?

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,387
Reaction score
4,880
Mpaka sasa dini ya haki imeshajulikana ni ipi neno HAKI ni neno hatari sana kwa watawala wanyonyaji, wauaji, wanyanganyi, wezi wa kura...nk

Hawataki kusikia msamiati haki ukitamkwa mbele za watu, mbele za watanganyika wapenda haki.

Kwa Tanganyika yetu ya leo ukijaribu kutetea haki wewe ni adui namba moja wa taifa hili, taifa hili linataka machawa na waongo tu.

Wanaomwabudu Mungu wa kweli watasimama na haki na kusema ukweli, baada ya viongozi wa kiroho wapenda haki kusimama na watanganyika vita vimeibuka juu yao.

Yupo wapi Gwajima leo, na leo Fr Kitima ameibuka kuwa adui wa watawala kisa neno haki na ukweli.

Viongozi wa serikali wameibuka na kuapa kupambana naye kisa kusema ukweli sio ajabu hata maisha yake yakawa hatarini, tukumbuke anaishi kwa neema za Mungu tu baada ya wauaji kunusurika kumuua siku za karibuni.

Vile vile kuna viongozi wa Kiislamu wao wanasema watachinja watanganyika ila uzuri wao huwezi sikia matamko yoyote ya kuwakemea.

Umefika wakati wa Wakristo kusimama na viongozi wao wa kiroho yasije kuanza kutokea ya Nigeria na huku.

Tuwaombee sana na kuwapa ulinzi kwa hata wakristo wenzao wamegeuka upande wa watesi.
 
Back
Top Bottom