Wakristo tujifunze kwa ndugu zetu Waislamu, wakati wa kufuturu unapata futari popote pale kwa urahisi bila bughuda, manyanyaso au kusubiri mwaliko

Hakuna Mungu ategemeaye juhudi za wanadamu! Hakuna.
Labda sikuelewa Uweza Wa Mungu?!
 


Wewe inaonekana ni mchanga sana kwwenye haya masuala ya kiimani.

Funga ya waislam ni tofauti kabisa na ya wakristo.

Kwa waislam, kufunga ni jambo public, ndiyo maana kwa baadhi ya mataifa, watu wanalazimishwa, na ukipatikana hujafunga, unaadhibiwa.

Kwenye ukristo ni tofauti kabisa. Kwa wakristo, suala la kufunga ni la siri, ni kati yako na Mungu wako. Na jambo hilo linatokana na maelekezo ya kwenye biblia:

Sikiliza Masiha Kristo anasema nini kuhusu kufunga, Mathayo 6: 16
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila ni Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

NB: Kwa imani ya kikristo, hata kama nimefunga, nikajinyima, kile nilichojinyima, natakiwa kumgawia mwenye shida, pengine bila ya mimi mwenyewe kujionesha au kujifahamisha mbele yake. Kama nitaenda kutoa hicho kitu mbele ya watu wengi ili nionekane nimetoa kitu kwa asiyejiweza, watu wakanishukuru na kunisifia, maana yake sina thawabu mbele ya Mungu maana nimekwishapokea thawabu ya shukranina sifa toka kwa wanadamu.

Na ufahamu kuwa wakristo wakati wa kwaresma, waanafundishwa kujinyima mambo wanayopendelea, wakati kwa waislam, mkazo upo kwenye kutokula mchana. Usiku wote ukitaka unaweza kuutumia kwa kula, na bado utahesabika umefunga.

Usipende kulinganisha imani ziinazotofautiana. Kama zingekuwa zinalingana basi sote tungekuwa imani moja.
 
Sasa kama umeshindwa kumsaidia mtu sahani ya wali ya buku 2 ndio utaweza kumlipia ada ya milioni?
Kwa nini umsaidie futari? Amesema ana shida ya futari? Nimesema pale mwanzo, acha kufikiria kula kula, kwamba una uhakika wa kufuturu! Haya sawa, mfungo ukiisha, utasaidiwa nini? Kupitia mfungo, tumieni hela mlizookoa kuwasaidia watu waliokwama katika jambo litakalowasaidia kuwapa msingi bora wa maisha, na sio kuwapa futari
 
Ni kweli imani zinatofautiana,ila yapo mambo ambayo wanafanana!
Embu tupe elimu kidogo,umesema kufunga kwa kristo ni siri,mbona kwaresma inajulikana wazi kuwa ni mfungo kwa wakristo,na wapo baaadhi wanafunga kila mwaka,siri iko wapi hapo? Au kwaresma haiko public kwamba kila mtu ana kwaresma yake?
Unasema saumu kwa wakristo ni siri, soma YOEL 1:14
"Toeni AMRI watu wafunge; itisheni mkutanno wa kidini. Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi, nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu" je kuna siri hapa"

Hivi yesu alivofunga mchana na usiku kwa siku 40 ilikuwa ni siri? Kama haikua siri hadi wewe umejua kuwa alifunga,je nayeye alikua mnafiki?
Je kuna mtu anaweza kufunga kama alivofunga yesu?

Uliposema kujinyima mambo unayoyapenda umemaanisha mambo gani kwa mfano? Na hayo mambo ni kwa mujibu wa nani? Maana SAUMU imeJe yesu mwalimu alivofunga alijinyima nini?

Hiyo hoja ya waislam kufunga ni kujinyima chakula tu wakati wa mchana umeitoa wapi? Kwanini uwazushie uongo?
Hao
Wewe unaona kujizuia kula mchana ni jambo jepesi, unayajua wanayotakiwa kufanya usiku waislam wakati wakiwa wamefunga?
Je,unajua wanavyotakiwa waislam kuenenda mchana wawapo katika mfungo?
Ni mekujibu kwa mtindo wa maswali maana umeonesha kama unaijua funga ya waislam mwisho unadanganya watu.

sikatai zipo funga za mtu binafsi mtu anaweza jifungia kwa siri kulingana na mapito yake,lakina Saumu za WAZI na za LAZIMA zipo kwenye dini zote!

Mwisho kila mtu ana dini yake,na imani yake,kilicho bora ni kuheshimiana na kuvumiliana,ila uzushi na ubaghazi juu ya imani ya wengine huzaa chuki tu,na chuki ni mlango wa shetani,chuki haina dini,
Zungumza unachokijua,kwa usichokijua busara ni kukaa kimya ujifunze ndio uzungumze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…