Mister mimi
Member
- Apr 29, 2018
- 89
- 106
Kivipi yani mkuu?
- M'moja anafunga , m'moja anabadilisha muda wa kula!
- Wana abudu "mungu" tofauti hawawezi fanana!
- Wana imani tofauti.
- Wana abudu Mungu na "miungu" tofauti!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kivipi yani mkuu?
- M'moja anafunga , m'moja anabadilisha muda wa kula!
- Wana abudu "mungu" tofauti hawawezi fanana!
- Wana imani tofauti.
- Wana abudu Mungu na "miungu" tofauti!
Wakristo wanafuturu?Mimi ni Mkiristo lakini nitumie fursa hii kuwapongeza sana Waislamu walio kwenye mfungo Kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa baina Yao na wengineo wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Ndio,wanaofunga wanafuturu,maana ya kufuturu ni kula chochote kwa mara ya kwanza tangu umenuia kufunga.Wakristo wanafuturu?
Wadau hamjamboni nyote?
Nasema Kwa dhati ya moyoni ndugu zetu ni wakarimu sana kutuzidi.
Mimi ni Mkiristo lakini nitumie fursa hii kuwapongeza sana Waislamu walio kwenye mfungo Kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa baina Yao na wengineo wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Kwao utapata futari bila kujali Imani yako au kuulizwa unakotokea tena bila manyanyaso au kuulizwa mwaliko
Ukweli wanatimiza amri ya upendo kikamilifu kama ilivyoagizwa kwenye Vitabu vitukufu
Ndugu zangu wakiristo tunamengi ya kujifunza kutoka kwa ndugu zetu Waislamu
Kwa nini umsaidie futari? Amesema ana shida ya futari? Nimesema pale mwanzo, acha kufikiria kula kula, kwamba una uhakika wa kufuturu! Haya sawa, mfungo ukiisha, utasaidiwa nini? Kupitia mfungo, tumieni hela mlizookoa kuwasaidia watu waliokwama katika jambo litakalowasaidia kuwapa msingi bora wa maisha, na sio kuwapa futariSasa kama umeshindwa kumsaidia mtu sahani ya wali ya buku 2 ndio utaweza kumlipia ada ya milioni?
Ni kweli imani zinatofautiana,ila yapo mambo ambayo wanafanana!Wewe inaonekana ni mchanga sana kwwenye haya masuala ya kiimani.
Funga ya waislam ni tofauti kabisa na ya wakristo.
Kwa waislam, kufunga ni jambo public, ndiyo maana kwa baadhi ya mataifa, watu wanalazimishwa, na ukipatikana hujafunga, unaadhibiwa.
Kwenye ukristo ni tofauti kabisa. Kwa wakristo, suala la kufunga ni la siri, ni kati yako na Mungu wako. Na jambo hilo linatokana na maelekezo ya kwenye biblia:
Sikiliza Masiha Kristo anasema nini kuhusu kufunga, Mathayo 6: 16
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila ni Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
NB: Kwa imani ya kikristo, hata kama nimefunga, nikajinyima, kile nilichojinyima, natakiwa kumgawia mwenye shida, pengine bila ya mimi mwenyewe kujionesha au kujifahamisha mbele yake. Kama nitaenda kutoa hicho kitu mbele ya watu wengi ili nionekane nimetoa kitu kwa asiyejiweza, watu wakanishukuru na kunisifia, maana yake sina thawabu mbele ya Mungu maana nimekwishapokea thawabu ya shukranina sifa toka kwa wanadamu.
Na ufahamu kuwa wakristo wakati wa kwaresma, waanafundishwa kujinyima mambo wanayopendelea, wakati kwa waislam, mkazo upo kwenye kutokula mchana. Usiku wote ukitaka unaweza kuutumia kwa kula, na bado utahesabika umefunga.
Usipende kulinganisha imani ziinazotofautiana. Kama zingekuwa zinalingana basi sote tungekuwa imani moja.