Wakristo tunaosheherekea 'Krismasi' Kesho kwa 'Yesu Kristo' Kuzaliwa 'Zizini' na 'Unyenyekevu' wake tunajifunza nini?

Wakristo tunaosheherekea 'Krismasi' Kesho kwa 'Yesu Kristo' Kuzaliwa 'Zizini' na 'Unyenyekevu' wake tunajifunza nini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kama huyu Yesu Kristo ambaye tunamsheherekea Kesho ( Krismasi ) alizaliwa Kimasikini Zizini ( Kraal ) ila bado akakubali Kufa kwa ajili yetu, anatuombea 24/7 na ni Mnyenyekevu asiye na Majivuno pia ni kwanini Sisi Wakristo akina GENTAMYCINE tumekuwa ni Watu wa Viburi, Jeuri, Nyodo, Maringo, Ubaguzi, Uchoyo, Kashfa na Roho Mbaya?

Tafadhali tulitafakari hili kwa Kina, tuombe Toba ya Kweli, tusameheane, tujisahihishe na Krismasi hii ya Kesho iwe ni Chachu Kwetu kubadilika Kitabia na Kimwenendo ili tumuishi Yesu Kristo kwa Matendo yake mema Kwetu na siyo maneno yetu matupu na Unafiki uliotukomaa hadi Akilini mwetu.

Naomba GENTAMYCINE niwe wa Kwanza kuwatakieni JamiiForums Members Wote Merry Christmas and Happy New Year. Mwenyezi Mungu atubariki Sote na tuendelee kuwa Great Thinkers hasa ambao tutakuwa Msaada mkubwa kwa Maendeleo ya Tanzania yetu na Rwanda yangu.

Mtakaoalikwa na Members Kesho kula Krismasi tafadhali ukifika muda wa Chakula usianze Kujipakulia bali subiria upakuliwe kwani hujaalikwa hapo peke yako na kama ni Kushiba utaenda Kushiba Kwako baadae kwa Kiporo chako ulichokiacha.
 
Swali zuri sana ndugu. Wakristo tunajifunza unyenyekevu, utu wema na zaidi upendo kwa watu wote na hasa kuwajali yatima, wajane na wagonjwa. Haya mambo Yesu Kristo ambaye alituachia tuyafanye kwa kumkumbuka siku zote.
 
Wajane tumesahaulika
 
Mimi Nina swali moja Kwa mleta maada,mbona huko mashariki ya kati kwenyewe alikozaliwa yesu na kukulia hamna hizo shamrashamra.
Naziona shamrashamra ni Ulaya,Ameriza zote,na Africa
 
Waafrika sjui mmelogwa na nani..
Huyo mnae msheherekea kesho hamjui hata tareh yake OG alizaliwa Lin, zaid ya stori za kusadikika, na tukiwauliza kwann mnatuita majina mabaya na kutuona wapinga Kristo[emoji23].

By the way Jesus never existed as real a man, mtadanganywa sana ndugu zangu kwa kushabikia dini ngeni.

Hiyo tareh 25 iliundwa tu na wajanja kwaajil ya kumuazimisha Mungu wa kale aitwae Zeus ama Krishna ama azazel ambaye baadae ndye huyo huyo alietumika kuunda kiumbe kipya kiitwacho Jesus ama yesu christo.

Kiuhalisia Hakuna ushahid wa uwepo wa huyo yesu, tafuta mahala popote pale dunian hutoona Shahid za uyo yesu wenu kuwa aliwahi kuwepo, zaid zaid utaambulia uongo wa kutungwa na mzungu hapo middle east kuwa aliish hapo miaka2000 iliyopita, wakat kiuhalisia miaka hiyo mahala hapo hapakukaliwa na hizo jamii za fake Jews, badara yake ilkuwa ardhi ya waafrika baadae ikaja kuwa ya waturuki na waarabu, sas huyo yesu wenu aliish wap?[emoji23][emoji23][emoji23].

Ukwel unauma sana Tena unauma Kama wew ni mshika dini na ukaambiwa ukwel usioujua, lazma tu utapinga.

Kutumia kitabu Cha biblia Kama reference ya ushahid uo ni upumbavu mkubwa maana biblia ni fiction book ambayo inakuwa updating kila Baada ya muda Fulani ili iendane na jamii ya kipind fulani.

Wakristo&waislam ni wakat wenu wa kujitafakari na kuanza kuchunguza Mambo ya Imani zenu kwa kuhoji na kutafakali hayo mliyokalilishwa na viongoz wenu.

Kuhoji si dhambi, Kuna mengi ndani ya maandiko yenu ambayo Kama yakiwekwa wazi naamini leo hii mtazikimbia izo dini zenu za uongo.

AMKENI!!...Muumba wa kwel hajawai na hatowai shuka dunian na hajawai na hatowai kufanana na mwanadamu kamwe..
huyo ibilisi wenu tokea middle east mtangoja sana kumsubiri na hatorudi ng'oooo kwakuwa hajawai kuwepo.
img_13_1617294394219.jpg
 
Mimi Nina swali moja Kwa mleta maada,mbona huko mashariki ya kati kwenyewe alikozaliwa yesu na kukulia hamna hizo shamrashamra.
Naziona shamrashamra ni Ulaya,Ameriza zote,na Africa
Hakuna sababu huyo yesu hakuzaliwa sehem Ile na wao hawamjui kwakuwa ajawai kuwepo zaid alitungwa na warumi miaka ya 325 b.c, na ninaposema bc namaanisha the age/period before christ, naposema Christ namaanisha ni kipindi ambacho mrumi aliunda karenda mpya ambayo ilitambulika Kama new age determined by the birth of ZEUS or Azazel and then Zeus huyo akaja kupewa jina jipya ili aendane na ustaharabu wa jamii za kizaz kipya ambaye ndye huyo huyo yesu/Jesus.

Tafuta sana maarifa ndugu, utajua Siri nyingi sana.
 
Noeli ni nini Kama si besidei!?..kwa hiyo Leo mnatuambia xmass sio kuzaliwa kwa Yesu?
 
hii siku na tukio lake na mtu aliyehusika sambamba na matendo yake, vinanipa picha kamili kwa hakika kizazi chetu kinahitaji matengenezo ili tuweze kuakisi matendo yake duniani kupitia ushirika usio na ukomo baina yetu na Mungu wa mbinguni.
 
Back
Top Bottom