SABABU ZA WAKAAZI WA MASHARIKI YA KATI KUHAMIA MAREKANI YA KUSINI KUANZIA MIAKA YA 1880
Andiko linatujuza kuwa si jambo geni kuhama kwa maelfu kwa hiyari. Andiko hili linafuatilia uhamiaji wa wahamiaji nusu milioni Waarabu kutoka Milki ya dola kubwa ya Ottoman Empire hadi bara la Amerika ya Kusini kati ya 1880 na 1914.
Wasyria, Palestinians, Israelis na Lebanoni wa milimani waliondoka Mashariki ya Kati ya enzi utawala ya dola ya Uturuki ya Ottoman iliyokuwa mtawala wa nchi za Mashariki ya Kati, ili kutafuta fursa katika uchumi unaopanuka wa kibepari wa ulimwengu wa Atlantiki baada ya azimio la kukomeshwa utumwa pande za Marekani ya Kusini.
Kupitia uhamiaji wa vibarua, Wasyria waliendeleza uchumi wa kimataifa wa kutuma pesa nyumbani Mashariki ya Kati kwa mafanikio makubwa na kufanya uwekezaji pembezoni wa Bahari ya Mashariki ya Kiarabu.
Usafiri wa maji, mawasiliano ya telegrafu, na teknolojia za uchapishaji ziliwezesha kuanzishwa kwa "koloni" za Syria (jalliyyat) huko Argentina, Brazili, na Marekani. Wakiwa nje ya nchi, wahamiaji wa Syria walijenga taasisi za kijamii ambazo ziliunganisha Bahari ya Atlantiki ya Kiarabu katika mabara na kuunganisha diaspora na nchi yao ya asili.
Jumuiya za kidugu, vilabu vya uhisani, jumuiya za misaada ya pande zote, na vyombo vya habari vya Syria vya diaspora kila kimoja kilichangia katika nyanja hii mpya ya umma, na kuchangia mafanikio ya kibiashara ya Syria pia kuvutia hisia za Vijana ya Kituruki nchini Turkey kufanya mapinduzi kuondoa serikali ya kifalme ya Ottoman ya Uturuki 1908.
Soma zaidi : Between the Ottomans and the Entente: The First World War in the Syrian and Lebanese Diaspora, 1908–1925. Stacy D. Fahrenthold, Oxford University Press (2019).
Video hii hapa chini kuhusu Waarabu wa jamii ya Amerika ya Kusini ambayo wengi hawajui historia ya wimbi kubwa la kuhama toka Mashariki ya Kati hadi bara la Marekani ya Kusini, Swali walifikaje na kwanini watu wengi hawafahamu ? Leo tutajadili ugeni mkubwa wa Walevanti wa Waarabu wa Lebanon, Syria na Palestina katika nchi za kisasa za Amerika ya Kusini, na jinsi Mashariki ya Kati ina uhusiano wa kihistoria na nchi hizi nyingi, kutoka Chile na Brazil, hadi Honduras na Mexico.
View: https://m.youtube.com/watch?v=XQsR0sDaSU8