Elections 2010 Wakristu na Waislamu kuiunga mkono CUF na kuipa kura za ndio ni baada...!

sokomoko,

..katika umri ule prof.lipumba hana mke?!!

..sasa hii itazusha maswali mengi mno, na kusambaratisha mjadala wetu.

..naona bora tujadili sera za cuf na ahadi anazotoa prof.lipumba.

hapa hatujadili habari za lipumba bali za kile jinachoitwa rais mtarajiwa padri slaa kuiba mke wa mtu na kumtambulisha hadharani kuwa ni mchumba wake!!!! Mimi sikujuwa kama ma padri huwa wanaruhusiwa kuwa na wachumba!!! Au ni sheria mpya? Lipumba hajawahi kusimama ktk mikutano ya kampeni na kumnadi mke wa mtu kuwa ni mchumba wake!! Bali ktk mikutano ya lipumba huwa tunasikia akinadi sera zake za elimu bure toka msingi mpaka chuo kikuu, matibabu bure nk, sera ambazo chadema wameziiba toka cuf!!!!

Sera za vyama vingine muibe!!!
Wake za watu munaiba!!!!
Sasa sijui kinachofuata ni nini?? Labda ni kuiba kura!!!!
 
Ukristo unaufahamu? basi kwa taarifa yako wakristu mwaka huu hawadanganyiki. Na askofu Kakobe kawafungua wakristo wengi macho. Wanajua nani wa kumpigia kura!
 

Hivi mbona hamjawahi kumuonyesha mke wa Prof hadharani...sio kwamba mnaogopa atawapunguzia kura katika ngome yenu kisiasa?

Please, acha kujidanganya...chama pekee chenye uhakika wa kura za watu wa dini zote ni CCM tu....hapo ndio mnapaswa kurudi nyuma na kuachana na siasa za short cuts...Wenzenu CCM na mapungufu yote na uozo uliokuwepo wanawashinda katika kutambua umuhimu wa kuwa sensitive na hisia za watu kijamii ziwe za kidini ama kikabila na hayo yao katika misingi ya chama chao kwa vitendo. Hata inapotokea wanateleza huwa hawachelewi kujirudi kwa staili mbalimbali sio wengine ambao mnajidanganya kuwa chuki na hisia za kidini ni mtaji wa kisiasa...
 
mod huyu anasemaje hapa?angalikuwa ms anagaliambiwa mdini?

MS sasa naona kuwa watu wanaosema wewe ni mdini wanakuonea. Wewe si mdini. Wadini hawafanyi haya uyafanyayo. Kinachokusumbua wewe si udini ni Utoto (Haijalishi una umri gani).
 
basi wazo zuri sema, wewe sio mdini ni muislam. kama mdini hata huyo mdini lakn kwa kuwa mkiristo wewe ndio umefurahia

MS, ukitoa hoja ya msingi yenye uthibitisho na manufaa haitajalisha kuwa wewe ni Muislamu ama la. Mkristo akitoa hoja ya kijinga ni ya kijinga tu. Nchi yetu ni masikini na sisi ni masikini pia, kupoteza muda kujadili hoja zisizo na tija ni kulikosea taifa letu. Tunaishi kama wachawi, JK akiwa madarakani tunaanza kuhesabu waislamu aliowateua mara Makamba, Kinana, Shein .... huu ni upuuzi! Mbona Wahindu hawasemi? Mbona wapagani na makafiri hawasemi? Wakristo na Waislamu tunalalamika kwa mema gani tuyatendayo? Huu ni upuuzi.

Mfano hii post ya Mwiba ina evidence gani? Niambie MS. Niambie. Tafadhali niambie.
 

Hizo habari zinaenea wapi?? Ukileta post JF hakikisha haina inatoa taarifa kamili. Tusaidie kujua, hizo habari zinaenea mtaani kwako, ofisini kwako au nyumbani kwako???
Li PUMBA kushinda uchaguzi ni ndoto kwa kuwa hata JK anajua kuwa mshindi ni Slaa (PhD). Maeneo mengi ya waislam kama Lindi, Mtwara, Tanga, Tabora na Kigoma JK na liPUMBA watagawana kura kwa kuwa CUF ina nguvu sana. CHADEMA watachukua maeneo yaloyobakia na kukomba za waislam wazalendo pamoja na wasomi. Tutajadili na kubishana sana hapa JF lkni mwisho wa siko mshindi ni Slaa (PhD)
 

Huu ndio udini. Kumbe tayari wengine mna wagombea wa waislamu na wa wakristo? Na hayo maeneo 'ya waislamu' na 'ya wakristo' ndiyo yapi? Msiwaharibie wenzenu. Mi ninavyowafahamu wagombea mliowataja ni wazalendo wanaoomba kura kwa wazalendo wenzao. Msiwapakazie udini wenu hapa!
 

Ndugu yangu hapa nakubaliana nawe kabisa. Kama kisa ni kuwa hakujua kuwa Josephine ni mke wa mtu, madhali sasa keshajua amwache basi atafute asiye na mume! Bado hataki! Sasa kama hicho si kiburi ni nini? Na je mtu kama huyo tukimchagua kuwa rais, mbona ni dalili wazi kuwa atakuwa mvunja sheria tena kwa kiburi, yani hata anapojua ni kosa bado hataki kujirudi.

Huyu mzee Slaa naona hata chembe ya aibu hana! Kama ni kweli tendo la kuchukua mke wa mtu lilitokana na kutojua, basi tulitegemea baada ya kujua ajirudi, amwache huyo mke wa mtu. Bado hataki! Ule utetezi wake umenichefua kabisa, na wakili mzoefu kama Marando kutoa utetezi wa kichefuchefu kama ule ni jambo la kushagaza sana!
 

Chuck it in the bin...absolute crap!
 

Ulichoweka hapa kinaitwa 'intellectual masturbation'! Ni uthibitisho gani ulionao kuwa Dr Slaa anazunguka na mke wa mtu? Kwako tuhuma ni sawa na hatia? Mlalamikaji amepeleka shauri mahakamani na huko atatoa ushahidi na mahakama ndiyo itakayotoa uamuzi kama kweli Dr Slaa kapora mke wake au la. Sasa wewe mtu tu wa nje usiyejua undani wa ndoa husika uanze kutuambia mambo ya 'moral na values'. Kwani 'moral na values' katika shauri usilojua undani wake ni nini?
 
Mimi simo kwani UZUSHI baba yangu alinikataza hata kusikiliza!!!!
 

Jamani muwe mnajadili hoja inayojitosheleza!

1. Mlalamikaji kapeleka shauri mahakamani kuwa Dr Slaa kapora mke wake na kumdhalilisha na anataka afidiwe kwa hilo.
2. Dr Slaa kakanusha kuwa hajwahi kumtambulisha mke wa mlalamikaji (kwa maana kwamba anayemtambulisha kwenye kampeni anaamini si mke wa mlalamikaji ni mke wake mtarajiwa).
3. Kwa hiyo, itabidi mlalamikaji apeleke ushahidi mahakamani kuonesha kuwa anayetambilishwa na Dr Slaa ni ni mke wake halali kwa sababu katika kesi za madai sheria inamtaka mlalamikaji athibitishe mahakamani kuwa anachodai ni kweli. Shauri hili halijatolewa uamuzi wa kisheria na hivyo Dr Slaa ana haki ya kuendelea kumtambulisha Josephine kama mke wake mtarajiwa mpaka mahakama itakapolitolea uamuzi tofauti au kuwa Joesphine ni mke halali wa mlalamikaji. Suala hili huwezi kulijadili hivihivi tu bila kuwa na uelewa wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inasema nini.
 

Mwandishi wa habari hii ameripoti kilichoandikwa kwenye 'statement' ya Dr Slaa ha hii post siyo 'copy' ya hiyo statement. Kwa hiyo, unapo'argue' ukumbuke kuwa un'argue' kuhusu mwandishi alivyoripoti na siyo kuhusu Dr Slaa alivyokanusha tuhuma. Pili, mlalamikaji kashtaki kuwa kaporwa mke. Dr Slaa kakanusha kuwa hajawahi kumpora mke. Je, kwa hao wawili kinachokufanya uhitimishe kuwa Dr Slaa kadanganya ni nini kama siyo 'prejudice'? Mimi nakushauri usubiri mahakama itoe uamuzi - kinyume na hapo Josephine ni mke mtajariwa wa Dr Slaa.
 

Fahamu tu huyo jamaa hajakurupuka tu na kwenda mahakamani ,ni baada ya kujua mkewe yupo wapi na nani na anafanya nini !! Upo ? Usimtete Slaa kwa kuwa ni mgombea wa Chama chako ,hapa kwa upande wangu sitazami chama nipo kwenye maadili na ubora wa kiongosi ,sasa kama wewe na wengine mnamtetea Slaa sijui mnamtetea kama yeye ni nani ? Ila kama ni wa chama chako sawa unayo haki hiyo ,kikamilifu kabisa ,ila uelewe kuwa maadili ya mtu ni kigezo bora cha uongozi ,Slaa kama Slaa amepoteza sifa hiyo kwa kuonekana hadharani akimtambulisha mwananmke fulani kuwa ni mchumba mtarajiwa ,hivi wewe kama wewe unaotaka kuposa au unapokuwa unachumbia ni lazima kuna masuala yatakutoka kumuuliza huyo unaemchumbia ,hivi ni kweli kuwa Slaa hakumuuliza ? chochote huyo mke mtarajiwa ? Alimsomba tu na kutokuwa na shaka au jambo lolte lihusianalo na maisha ya kabla ya kukutana ?

Habari za karibuni zinasema Slaa amesikika akisema kuwa hakujua kama huyo ni mke wa mtu ? Hivi inaingia akilini ,na kama hakujua basi alidanganywa na hakuna wa karibu yake aliekuwa akimjua huyo mwananmke ? Ndivyo Slaa anavyotaka kuueleza umma. Mdai hakuwahi kumwacha huyo mwanamke ,sasa hata kama imepita miaka mia basi bado ni mkewe ,iwe huyo mwanamke amewahi kupeleka malalamiko mahakamani ,hapo pia patahitaji uamuzi wa huko alikopeleka malalamiko. Kama haitoshi huyo mwananmke alikuwa na watoto ,bila ya shaka Slaa aliwahi kuwaona na kuhoji kama hakuwahi bado atakuwa anafichwa ,kama ni mtego basi Slaa ameuingia kichwakichwa .mpoo ?
 
Hajui maana ya ndoa. aliyekwambia Dr.Slaam kachukua mke wa mtu nani? anatuhumiwa! hivi tukianza kuhalalisha tuhuma na kuhukumu kwa kutumia tuhuma kuna mtu wa ccm atakayebaki salama? Usifikiri kwa kutumia nyayo!!!
 

kama tuhuma si hatia mbona chadema munapiga kelele jk kuwakampenia mramba NA WATUHUMIWA WA KESI YA UFISADI? Wao si ni watuhumiwa? Na kesi zao ziko mahakamani? Sasa kama slaa anatuhumiwa kubaka mke wa mtu si kosa basi na jk kukampeni kwa mramba na lowasa pia si kosa!!!
Upo hapo? Au mkuki kwa nguruwe.........
 
post ya kwanza unakuja na hasira kama umenyimwa tshirt na kofia ya njano. tulia, kabishe hodi kulee!
 

Interesting.

Linapokuja suala la "mafisadi papa" wa CCM, Kikwete anavikwa dhambi za kutowachukulia hatua. Akisema kuwa hawezi kufanya hivyo hadi mahakama itoe hukumu mnasema amekumbatia na anaogopa mafisadi. Sasa hivi mnatetea suala la Slaa na "mke wa mtu" kwa style ileile ya Kikwete cum CCM na Mafisadi Papa....

Halafu u still dare kuongelea ukombozi wa Tanzania upo mikononi mwenu. Huu unafiki unatia kinyaa. Now I start to agree na Kikwete kuwa vyama vya upinzani ni foto kopi yao.

Ote dugu moja.....

Nawashauri mjaribu kufocus campaign/propaganda zenu katika kutoa hoja za maendeleo kama zipo na kuacha huu unafiki wa kuhalalisha ama kuchakachua uozo.....mengine myanyamazie tu kuliko kutumia nguvu hata za watu wanaopaswa kutukanya maovu wafanye kazi ya kuhalalisha maovu....
 
Nnachowapendea humu ni kwamba wanamtetea Slaa kwa gharama yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…