Wakristu tumebipiwa na shetani naomba tumpigie kwa sherehe kubwa tufufuke na kristo

Wakristu tumebipiwa na shetani naomba tumpigie kwa sherehe kubwa tufufuke na kristo

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema!
Kipindi cha kwaresma huwa ni kipindi cha kuyatafakari matendo makuu ya Mungu!
Wapo wanadamu wanaothubutu kujitwalia utukufu wa Mungu! Lakini kamwe Mungu atabaki kuwa Mungu na wala hachunguziki!

Skukuu ya pasaka ni siku ya furaha kubwa ya ufufuo wa Yesu kristo!

Siku hiyo lazima kila mkristo ashangilie ufufuko huo kama alama mkombozi!

Kuna tamko limetolewa na wanaojiita wanamamlaka ya kupiga marufuku watu kusherekea pasaka!
Hawa ni sawa na yule pepo mchafu!
TUWAKEMEE KWA JINA KUU LA YESU KRISTO!

Ikumbukwe yule pepo mchafu yupo anaishi Hapa duniani kupitia nafsi za watu waliohai!
Watu hao wanathibitika kwa tabia ya ushirikina, matamko au hata matendo yao kuwa kinyume na mapenzi ya Mungu.

Watu hawa tunaishi nao humu duniani wengine wananafasi za kimamlaka katika inchi!

Yaani Kristu aliyefufuka tuache kumuimbia ALELUYA KWA SHANGWE! Eti kisa mwanadamu?

Tena mwanadamu Mwenyewe anasubiri kuja kufufuliwa na kristo siku ya mwisho?!

Aliyetoa hilo tamko la kuzuia sherehe ya pasaka siyo mtu sahihi nazani ni pepo!
Wakristo huu ndiyo mda wa kumtangaza kristu aliyefufuka kwa vitendo!

WATAKE WASITAKE TUTASHANGILIA UFUFUKO WA KRISTO KWANZA!!!

Na tuwaombee kwa Mungu viongozi wanaotoa matamko kama hayo mapepo yawatoke!!
Kwasababu hawana tofauti na waliomtesa YESU! Kwa kumsujudia BARABA!
 
Back
Top Bottom