Wakristu wenzangu, nyie mnaombaje hadi kujibiwa maombi yenu. Tusaidiane kwa mapenzi ya kristu

Wakristu wenzangu, nyie mnaombaje hadi kujibiwa maombi yenu. Tusaidiane kwa mapenzi ya kristu

Cha kwanza MUNGU ni MWAMINIFU sana

Usikate tamaa mtumish
Don't give up the servant

Endelea kuomba na kuombea unachokiombea

Lakin pia MUNGU halazamishwi kwa mawazo yako wewe muombaji

Yeye mwenyewe atatenda kwa wakati wake endelea kusali mtumish
 
Tataizo yenyu ni kwamba mnadhani kumuamini mungu basi hutapitia magumu ya maisha...
kama aliruhusu yule jamaasijui nuhu ajaribiwe kwa sharti tuu kuwa shetani asimtoe roho inamaanisha kuwa binadamu ata uwe na imani kali majaribu ya maisha utayapitia tuu.

Muhimu ni kuendelea kumuamni mungu na kuishi vile amethelekeza tuishi. Mfano rahisi hao mataliban sii wanamuamini mungu lakini umeona jinsi imebidi wapigane vita miaka 20+ ili kufikia jambo lao.
 
Tatizo tulilonalo waumini wengi ni kuwa tunaomba tu pale tunapopitia hali fulani na sio utaratibu wetu kuomba hata tukiwa kwenye hali ya kawaida.

Si unaamini katika ukristu? Kwa waaminio Mungu huwa hachelewi wala hawahi kujibu maombi yako, hujibu kwa wakati sahihi. Uo wakati sahihi hatujui ni lini na saa ngapi kwahiyo inahitaji uvumilivu kwa unalolitegemea. Zingatia kwa waaminio.
Dini na siasa havina tofauti.

Eti Mungu hawahi wala hachelewi- hii ni nadharia ya uongo na bahati na sibu. Ili mambo yakienda mlama uambiwe hawahi, yakija kwa bahati tu uambiwe hachelewi😅😅😅
 
Imani....hata bila kuvuja jasho kwenye maombi ukishakuwa na Imani unatoboa....
Kuingia faragha na kuanza kuomba ni ishara ya mtu mwenye Imani na Mungu kuwa Ndiye Mwokozi uyu anahitaji mafunzo zaidi unajua unapoingia katika wokovu unakuwa Jeshi lakini la mgambo na yeye anahitaji kuwa mwanajeshi kamili mwenye mafunzo

Shida nyingine kwa wakristo wengi huwa wanaomba ili wapate mafanikio
Lakini Mungu wetu kabla hajampa mtu mafanikio huwa anaachilia ufahamu wako ili ujue kwanini haufanikiwi anaachilia ufahamu wako ili ujue unakosea wapi hivyo unahitaji kuwa na nguvu ya Roho Mtakatifu ndani yako ili uwe connected kwa kupewa majibu Nini ufanye
Bila Roho Mtakatifu huwezi kufanya lolote
 
Nimefunga, nimeshirikisha, nimeomba alfajiri lakini bado tabu ninayopitia inaendelea kunitafuna.

Tusaidiane wakuu.
Usihofu Mungu bado yupo pamoja nawe upo kwenye njia sahihi haijalishi hali unayopitia

1 Wathesalonike 5:17-18,24
[17]ombeni bila kukoma
[18]shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
[24]Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.

Lakini mpendwa shida yako hausomi biblia kuomba bila kusoma neno ni sawa na mwanafunzi anayeingia kwenye chumba mtihani bila kusoma semester nzima unategemea miujiza gani hapo soma biblia kila siku mara tatu

Yoshua 1:8
[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
 
Nimefunga, nimeshirikisha, nimeomba alfajiri lakini bado tabu ninayopitia inaendelea kunitafuna.

Tusaidiane wakuu.

Hakuna aliyewahi kufanikiwa kwa huo UTAPELI wa MAOMBI...

Yangekuwa yanafanya kazi this world would have been a very different place...
Wale wanaokufa pale OCEAN ROAD na MLOGANZILA nao wanayajua hayo maombi...
 
Nimefunga, nimeshirikisha, nimeomba alfajiri lakini bado tabu ninayopitia inaendelea kunitafuna.

Tusaidiane wakuu.
Tabu gani unayopitia mkuu kwa maana si kila tabu inatatuliwa kiroho moja kwa moja ila kuna tabu kabla hazijatatuliwa kiroho ni lazima zitengenezewe mazingira yanayohitajika ili kutengeneza uunganifu kati ya huo ulimwengu wa kiroho hadi kwenye ulimwengu wa damu na nyama ambako ndiko hiyo tabu yako inakopatikana.

Nikutolee mfano tabu ya kifedha, hii ni moja ya tabu ambayo unaweza kuomba hadi ukagalagala chini lakini kamwe huwezi itatua kiroho moja kwa moja kama hautaitengenezea mazingira ya kuiunganisha ile njia inayopokelea hayo maombi au baraka kutokea upande huo wa kiroho kuja moja kwa moja kwenye upande wa damu na nyama.

Na matatizo mengi ambayo huwa ni ngumu kuyaombea moja kwa moja ni yale ambayo tayari mtu yalikuwa ndani yake tangu ile siku anazaliwa ila yanaenda tofauti kwakua yeye mwenyewe anaenda kinyume na misingi au nje ya njia zile ambazo mambo hayo hupita kwa hiyo mtu hujikuta anapishana nayo yeye mwenyewe kwa hiyo kwa namna hii hata uombe vipi hutoweza kutatua tatizo hilo ila utatatua hilo tatizo pale tu utakaporudi kwenye misingi au kupita kwenye njia zake na baada ya hapo ukifanya maombi yanapopita kwenye hizo njia yanakutana na wewe moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom