Wakubwa Naombeni Msaada wa Mawazo Yenu.

Wakubwa Naombeni Msaada wa Mawazo Yenu.

Wakuu shikamooni..Leo sitaandika kwa ile Lugha ya Kiarusha(Ngareroo slang)Kwasababu Nna jambo naombeni msaada wa mawazo yenu kama kaka zangu na Dada zangu,,So leo naomba niandike kwa lugha inayoeleweka ili mnisaidie mawazo na Asipatikane mtu wa kusema hajaelewa hii ni kutokana na watu wengi humu kudai hawaelewagi wengine pia husema bangi,uhuni na maneno kibao...Naam hapo,Nna msichana tunaishi nae uku Arusha japo yeye anakaa Kikatiti mimi nipo apa Kijenge juu,Huyu binti ana umri wa miaka 19 na kwasasa yupo Mwanza kimasomo,Nakumbuka mahusiano yetu yalianza mwaka jana mwezi wa6,Na hadi kufikia hapa tushawekeana malengo kabisa ya kuoana coz anakila sifa nnazozihitaji za kuwa mke wangu,Ndo mwanamke nnaempenda kuliko wanawake wote duniani ukimtoa Mama angu,Dada zangu anafata yeye then Cardi B,kiukweli ananipenda sana kunizidi hata mimi navyompenda,yaani nikimkosea kidogo tu analia,Nakumbuka kuna siku nilimtania tuachane tubaki marafiki,alilia sana hadi marafiki zangu wakanisaidia kumnyamazisha,Kila akirudi likizo home anakuja na zawadi zangu,pia nakumbuka semester iliyopita alinilipia nusu ya accommodation fees(ada ya hostel)alitoa laki na nusu alimdanganya Baba'ake sijui wana study tour ya Wapi?Then nusu nikamalizia mimi ikakamilika laki3,,,Sasa bwana huyu dem kuna namba yake ya voda alinambia nimtumie video3 WhatsApp,Tamu ya Mbosso,Roboti ya Whozu na Tetema ya Rayvanny na Mond,Basi nikamtumia lakini alisema bado hajaziona coz alikua hana bando ila akasema akiweka ataziona,huyu dem yuko shule na hutumia sim ki'sirisiri coz haziruhusiwi,,Sasa siku mbili baadae akanambia ile namba niifute na nisiitumie kabisa coz simu ilikamatwa alaf yule mwalimu akaichukua laini then akaichukua namba yangu akaiandika kwenye karatasi coz alikuta imeseviwa"My husband"yule ticha akasema atanitafuta kisha akai'block ile laini akamrudishia dem,dem alipoona ime'blockiwa akaamua kuivunja tu kwa mujibu wake alivosema,,,Kweli mimi nikaifuta ile namba but juzi kuna namba ngeni Ikanitumia sms ikinipiga biti kuwa niachane na uyo manzi,mimi nikajua labda kakosea namba chalii,nikamuuliza Manzi gani?akanitajia jina la dem wangu kabisa alafu akazitaja na video zilezile nilizotuma daah..!!Chalii kanitukana sana anadai hiyo namba aliachiwa na uyo dem na akaambiwa eti atutukane washkaji wote tunaomsumbua,Basi bhana nikamkaushia yule jamaa ikabidi nimuulize dem aliponitafuta ile jana kwa simu na namba ingine,Dem kakana hamjui chalii na hajui iyo namba'ake kaipataje!Dem kajitetea hadi akaanza kulia kazira hadi kula wanafunzi wenzake wananambia,,Ila yule jamaa nimeongea nae kistaarabu.kasema ameamua kuniachia niendelee nae coz nna malengo nae,,,Wakuu zangu nnachowaomba mnisaidie Je huyu dem kweli hamjui uyu chalii na ananipenda kweli?yule chali nilimuuliza namba'angu kaipataje?akasema alizipata WhatsApp nilipotuma zile video coz nilifikiri ndo yule ticha aliechukuaga laini ila sio coz uyu ni kijana tu mdogo na yuko Form4 apa Arusha sec.so sio yule ticha,,Nisaidieni wakuu nifanyaje ili niujue ukweli istoshe dem saiv yuko so disappointed kinyama na wana mitihani walianza jumatano naona kabisa hatafanya poa,,,,Asanteni sana.
@ChaliiYaKijengeJuu.
Mkuu usiweke malengo hapo bado mdogo huyo , ila kama unaweza himili maumivu yake wekeza

Wolf nation
 
Kama kakuruhusu mwenyewe kusafisha rungu endelea kusafisha rungu ila malengo ya kuoana hapo mnadanganyana umri wenu bado mdogo sana kuanza kuwekeana malengo makubwa hivyo mimi mwenyewe na utu uzima wangu bado naonekana sijapevuka bado na nina miaka 24 sembuse nyie miaka 19kwa 22 hamko serious
 
MREJESHO WA THREAD:Wakuu napenda kuwashukuru wote mlionipa ushauri kadri mlivyoweza,,Naam katika mrejesho hatimae leo rafiki ake kanitafuta anasema siku ile tuliyoongea nae hadi akalia presha ilipanda akapelekwa hospital na leo wameachiwa anaendelea vizuri ila yeye bado sijaongea nae alikua kalala.
 
Mangi jua tu kuwa ni mapema sana kumuamini mwanafunzi especially aliyeko bado secondary school. Hapo bado hajaenda chuo akawa huru kufanya atakacho tena bila ya usimamizi wa yeyote. Perhaps huyo ndio first love wako na sitaki kukukatisha tamaa lakini ukweli ni kwamba huyo Ngachude atakuzingua mbeleni.
 
chali kwema?

naomba nitangulize pongezi kwa kuomba ushauri ni jambo la busara sana kwa age yako kutaka mwanga juu ya swala hilii...naona hapo dem 19,wew 21..ni umri sahihi kabisa kupitia hisia hizo za ki real moyoni kabisa yani...

ukweli wa mambo wadau wengi hapo juu sio kwamba wanasema kwa ukali au kwa kukubeza kwamba umri bado mtaachana nk. ila ni kwasababu hiyo ni stage kila mtu akikuwa lazma apitie...mkitoka hapo mtaweza jikuta mkaa hata miaka saba pamoja ya u bf na gf..ila huyo akianza fika umri flani 26-29 au karibia na huko atapata phase nyingine kabisa ya ndoa na kutamani vitu vingine sasa hapo anakutana na mabloo 30-37 nao wanamihemko ya ndo ndo wanapo kutana..nawew umri huo sasa utapata kidem sasa 19-22 kipo real kinakuelewa sana kwasababu wewe umepitia huko utakivutia kasi nakukiambia tulia maliza shule nk ntakuoa tu kwasababu nawew umepitia huko sasa kakitulia miaka 25 wewe nawew una kuwa 32 nk umejipanga unatia ndani..

hizo ni hesabu kwa asilimia kubwa na ukweli ulivyo..ndo mana wanakushauri hapo juuu usiumize saaaana kuwaza kama ankupenda jua anakupenda nawe unampenda ila muoneshane upendo akiwepo nk.akiwa shule mjengee mazingira atulie akumis wewe upo na akirud mtaonana...maana anapopata nafasi ya mawasiliano anaacha kuwatafuta walipa ada anakutafuta wew ambaye kimsingi huna msaada wowote maans hapo ata hostel alikusaidia unakuws unashusha nguvu yako kama chaliii yan wakiume...dem acha akumiss acha uadimike ase...utamjengea mazingira akukwepe maana anajua hakawii nililia shida na vijana nawajua hapo kila ukiongea nae baada ya mda unamjengea mazingira ya kibom😂..nakutania ila natumai umeelewa nachotaka kukuelewesha .tulia mle penzi akiwepo akiwa shule tuliza hisia ...
 
Back
Top Bottom