Wakubwa tunawakumbusha kuhusu ile tume ya ku-harmonize mishahara

Wakubwa tunawakumbusha kuhusu ile tume ya ku-harmonize mishahara

Mkyamise

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2014
Posts
482
Reaction score
614
Nakumbuka kuna tume hii ambayo ilipigiwa chapuo na wakubwa wa government kuwa ndio itakayokuwa suluhu ya tofauti kubwa ya mishahara katika utumishi wa umma. Je hii tume mpaka leo haijakamilisha kazi yake?
 
Mkuu pambana upate kipato halali nje ya salary mengine potezea
 
Saivi tume ni ya mtu mmoja kama unabisha chunguza wale watumishi waliolimwa panga la mishahara kama wiki mbili zilizopita kwa tamko tu la mtu mmoja.

Turudi kwenye mada. Tume unayozungumzia ilikufa kifo cha mende lilipo ingia swala la uhakiki vyeti feki watumishi hewa, NIDA n.k

Nakumbuka swala hilo liliimbwa ndani ya mwaka mmoja tu na kisha lijapotea/potezwa
 
Kumamae umenikumbusha aseee ngoja niwahi ikulu nikamkumbushe mzee.....Kama mbwai na iwe mbwai
 
Mkuu pambana upate kipato halali nje ya salary mengine potezea
Hata hivyo vipato vinavyoitwa vya nje, ukichunguza utakuta navyo ni salary. Lakini pia wapo wengi waliolizwa na jamaa au wasimamizi wa miradi yao ya nje kwa kushindwa kugawanya muda katika kudeal na kazi zao za ajira vs miradi yao ya nje
 
Ilikuwa changa la macho,we,endele kupambana na hali yako ndugu
 
Miongoni mwa Vitu vinavyoondoa Uzalendo kwa Wananchi wengi ni hii tofauti kubwa ya mishahara kwa watu wenye fani sawa,kiwango cha elimu sawa na hata uwajibikaji nao unalingana lakini mwisho wa mwezi kuna mtu anachukua Mlima Kilimanjaro, mwingine anaondoka na kichuguu. Wala sio kweli kwamba watumishi wa TRA wanafanya Kazi nzito kuliko watumishi wengine au wanaofanya Kazi katika mashirika ya Umma, Serikali iliahidi kufnaya urari/harmonization ya package na ifanye hivyo sasa bila kizingizio chochote kwa sababu Katiba yetu ibara ya 9 na 13 zimezuia kabisa ubaguzi wa aina yeyote kama wa rangi,kipato, elimu au mahali pa kufanyia Kazi.
 
Back
Top Bottom