Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Wakulima wanahali mbaya kuzidi hata enzi za mkoloni. Uhuru wao bado kufika.
1. Wakati wa mkoloni kulikuwa na bodi za mazao, lengo lake ilikuwa ni kupanga bei na kumnyonya mkulima. Tulipopata uhuru zikaendelea na kuwekwa kitu kingine kinaitwa vyama vya ushirika. Hivi vinanunua mazoa kwa bei ya chini halafu vinauza nje na kisha vinapiga faida. Bei ya dunia ya mazao inaweza kupanda lakini vyama hivi havipandishi. Gharama za uzalishaji zinapozidi kukua watu wanaamua kuacha kulima au kuuza kwa magendo. Kama wakulima wa kahawa Kagera.
2. Mkulima ndiye mtu ambaye hana uhuru auze wapi matunda ya jasho lake. Hana uhuru huo kabisa. Serikali inamlazimisha kuuza kwa vyama vya ushirika nk, na kwa wale wa chakula imekuwa ikifunga mipaka.
3. Mkulima ndiye anayelipa madeni ya nchi lakini siye anayefaidika na mikopo hiyo. Serikali inakopa pesa na kujenga hospitali, barabara za lami, mifumo ya maji nk maeneo ya mijini. Lakini watu hawa wa mjini hakuna wanachozalisha kikaingiza pesa za kigeni kulipa madeni, kama kipo ni kidogo mno. Nchi inategemea kuuza kahawa, pamba, korosho, chai nk ili kupata pesa za kigeni kulipa madeni. Hivyo aneyefaidika na mkopo halipi na anayelipa hafaidiki nao.
Mkulima bado hajawa huru.