Wakulima hutumia 24% ya kipato chao kununua GB 5 za data

Wakulima hutumia 24% ya kipato chao kununua GB 5 za data

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Hali ni mbaya kwa ununuzi wa data kwa wakulima. Kwa takwimu za NBS za 2020 wakulima wanapata kwa wastani Tsh. 169,377 kwa mwezi. Wastani wa fedha wanazopata wanawake ni ndogo zaidi kuliko wanaume ambapo wanawake huingiza kwa wastani Tsh. 124,479 na wastani wa wanaume ni Tsh. 195,617.

Kwa Takwimu za TCRA MB moja kwa robo ya mwisho ya mwaka 2022 iliuzwa kwa Tsh 8. ambapo GB moja ni sawa na Tsh. 8192 ambapo GB tano zinakuwa ni Tsh. 40960

Kwa bei hizo maana yake kwa kila mwezi wakulima hutumia 24% ya kipato chao kununua walau GB tano za data. Hali hii ni kuwa watu hawa wanakutana na fursa finyu za mtandaoni.

MaleFemaleTotal
195,617​
124,479​
169,377​
GB tano kama wastani wa kipato
21%​
33%​
24%​
Ikumbukwe kuwa wanaopigania unafuu wa bei za data wanashauri GB tano ziuzwe kwa bei ambayo ni chini ya 2% ya kipato cha mtu. Hii inaonesha gharama za data ni kubwa sana kwa Tanzania


Kwa waajiriwa wa makundi mengine,

MaleFemaleTotal
Paid Employees
396,885​
378,469​
390,992​
5GB as ratio of Income
10.3%​
10.8%​
10.5%​
Self Employed
420,288​
233,918​
327,057​
5GB as ratio of Income
9.7%​
17.5%​
12.5%​

OLS
 
Back
Top Bottom