Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Maswa, Simiyu: Wakulima wa pamba wilayani Maswa wameonywa kutokubali kuuza pamba kwa mkopo, bali wahakikishe wanalipwa fedha zao mara moja baada ya kukabidhi zao katika vituo vya ununuzi.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Maswa, Lukas Kuwingwa, amesema taasisi hiyo iliingilia kati baada ya wakulima wa Jilago kulalamikia kucheleweshwa malipo ya pamba waliyouza kupitia AMCOS ya Jilago kwa Kampuni ya Alliance Ginner.
Jumla ya Sh10 milioni zilidaiwa na wakulima 25, huku TAKUKURU ikihakikisha fedha hizo zinapatikana na wakulima kulipwa.
Afisa Ushirika Wilaya ya Maswa, Godfrey Mlanda, amewataka wakulima kutokabidhi pamba iwapo fedha hazipo katika vituo vya ununuzi.
“Uza pamba yako upate pesa yako, usikubali kukopwa.”amesema.
Baadhi ya wakulima waliopata fedha zao, akiwemo Yunice Emanuel, Kwilasa Bundala, Gulasa Masunga na Silya Ntemi, wameishukuru Serikali kupitia TAKUKURU kwa kuingilia kati na kuhakikisha wanapata malipo yao.