Vyama vikuu sita (6) vya wakulima wa mikoa minne (4) inayolima Korosho kwa wingi hapa nchini wamesema wanatarajia kutoa shilingi milioni 11 ili kumchukulia fomu Rais Samia Suluhu Hassan ya kugombea nafasi ya URais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani (2025), ambapo watamchukulia fomu hiyo pindi muda utakapofika, sambamba na kumuwekea mafuta kwenye gari lake wakati wa kampeni kwa kumshukuru kwa aliyowafanyia wakulima wa korosho katika utawala wake.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Wakulima wa mkoa wa Pwani (CORECU) Musa Mng'ereza amesema hayo kwa niaba ya Wenyeviti wenzake wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Rufiji, mkoani Pwani ambapo amesema, "kwa mapenzi yao wakulima wa korosho wa maeneo hayo wameamua ifikapo mwaka 2025 watamchangia pesa ya kuchukua fomu na pesa ya mafuta".
Amevitaja vyama vitakavyoshiriki kuchanga fedha hizo kuwa ni pamoja na CORECU, RUNALI, Lindi Mwambao, TANECU, MAMCU na TAMCU vyama kutoka mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma
Source Jambo tv
Umasikini ni mtaji mkubwa sana wa CCM, Na CCM hawako tiyali kuona umasikini unaisha katika Taifa hili. Hao wanao changa pesa ukifika kwao ndio utajua what is Poverty.
SIo elimu, shida ni umasikini unao sababisha raia waone kila kitu ni zawadi kitoka kwa Watawala, yaani Mfano mvua zikaanza kunyesha mapema huko kwenye mashamba ya korosho wao wanajua ni sababu ya watawala. Na umasikini ni mtaji mkuu namba 1 wa CCM
Umasikini ni mtaji mkubwa sana wa CCM, Na CCM hawako tiyali kuona umasikini unaisha katika Taifa hili. Hao wanao changa pesa ukifika kwao ndio utajua what is Poverty.
Unachanganya umasikini na ujinga au elimu duni.....inataka kumanisha kwamba Kenya hamna umasikini au Uganda wanaunafuu kutuzidi, kinacho sumbua nchi yetu ni elimu duni na unafiki.