Wakulima wa mbegu za vitunguu, wauzaji pamoja na wanunuzi tukutane hapa

kido madini

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
223
Reaction score
144
Wale wakulima wa mbegu za vitunguu (baruti) wauzaji pamoja na wanunuzi tukutane hapa.

Nadhani hii itakuwa ni sehemu sahihi kabisa ambayo itamrahisishia mkulima kujifunza na kutoa uzoefu wake katika kilimo hiki ambacho watu wengi bado hawajakipa kipaumbele ingawaji kilimo chenye faida kubwa sana katika kipindi cha siku 120 hadi 140
pia naomba mods msiuunganishe uzi huu kwenye uzi mwingine

pia kwa wale wakulima ambao wanatafuta mbegu hizi za vitunguu kwa ajili ya kilimo cha kitunguu cha kawaida itawarahisishia kuuunganishwa na wazalishaji wa mbegu (baruti)
 
Nipo hapa,Mimi nataka kulima kitunguu nimeandaa eka mbili za mbuga.
Kwa sasa nataka niangushe shamba na nitapitisha tena jembe LA tractor afu ndo nitapanda!
Ndani ya eka mbili hizo naweza vuna gunia ngapi?
Mbegu sijapata pia.
 
Ndani ya ekari mbili wastani wa mavuno ni tani 10 mpk tani 12 km una chembeka yani umepanda kwa vitalu lakin km unapanda broadcasting yani unamwaga hizo ekari mbili utapanda wastani wa debe moja na nusu hadi debe 2 mavuno ni gunia 50 hadi 70 kwa ekari moja
 
Ndani ya ekari mbili wastani wa mavuno ni tani 10 mpk tani 12 km una chembeka yani umepanda kwa vitalu lakin km unapanda broadcasting yani unm. amwaga hizo ekari mbili utapanda wastani wa debe moja na nusu hadi debe 2 mavuno ni gunia 50 hadi 70 kwa ekari moja
IPI inaleta mavuno mazuri kati ya hizo njia mbili za kupanda?
 
Naomba kufahamishwa hali ya hewa ambapo vitunguu vinaweza kustawi vizuri,,nimehamia mkoani Njombe wilaya ya makete,vipi kwa hali ya hewa(baridi mno) ya huku vitunguu vinaweza kustahimili vikamea vizuri?
 
NDIO VITUNGUU HUSTAWI KWENYE HALI YA UBARIDI INGAWA Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo

nakushauri kama huko kuna vyanzo vya maji ya kutosha lima kipindi ambacho mvua zinaenda mwishoni ili uwe una mwagilia
sababu naskia huko mvua ni nyingi na kama ni nyingi utaozesha mali maana vitunguu havitaji maji ya kuzidi na ukizingatia sikuhizi tunalima mbegu hizi chotara hazipendi mateso
 
Asante sana,mvua ni nyingi na udongo ni mnyevu pia.
Mfano,nimekuta wanalima mahindi kipindi chote cha mwaka bila kumwagilia pia bila mvua nikashangaa sana.

mmebarikiwa na bwana sie huku singida ingekua hivyo tungeilisha tanzania
 
Nipo hapa,Mimi nataka kulima kitunguu nimeandaa eka mbili za mbuga.
Kwa sasa nataka niangushe shamba na nitapitisha tena jembe LA tractor afu ndo nitapanda!
Ndani ya eka mbili hizo naweza vuna gunia ngapi?
Mbegu sijapata pia.
Muone huyu jamaa ana mbegu nzuri sana.

Nauza mbegu ya vitunguu.
Mbegu ni RED MANG'OLA au nyekundu zambarau
Nipo Singida ila popote nchini inafika
BEI ni Tsh 350,000/= kwa ndoo kubwa mfuto.
Tsh 400,000/= kwa ndoo kubwa kichuguu
Maongezi yapo call 0625887645/0754710051
 
Ndani ya ekari mbili wastani wa mavuno ni tani 10 mpk tani 12 km una chembeka yani umepanda kwa vitalu lakin km unapanda broadcasting yani unamwaga hizo ekari mbili utapanda wastani wa debe moja na nusu hadi debe 2 mavuno ni gunia 50 hadi 70 kwa ekari moja
Tone 1 average unaweza ukauza sh ngapi
 
Mi nalima Njia panda Moshi nashukur sijawahi Pata hasara
 
Muone huyu jamaa ana mbegu nzuri sana.

Nauza mbegu ya vitunguu.
Mbegu ni RED MANG'OLA au nyekundu zambarau
Nipo Singida ila popote nchini inafika
BEI ni Tsh 350,000/= kwa ndoo kubwa mfuto.
Tsh 400,000/= kwa ndoo kubwa kichuguu
Maongezi yapo call 0625887645/0754710051
Ndoo kubwa inatosha kupanda acre ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye kuhitaji mbegu ya kitunguu anicheki
 
Back
Top Bottom