SEAL Team 6
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 655
- 118
Tangazo lililotolewa na Serikali la kupandisha bei ya zao la Pamba nchini kwa musimu huu, kumbe ilikuwa ni kuwapa matumaini hewa. Tangazo hilo lilitolewa Kasulu bei ya pamba ingekuwa ni sh.1,100/= kwa kilo, Waziri Mkuu juzi Bungeni alikana live na kufuta kauli hiyo ya Serikali na kuwataka WANUNUZI wa Pamba wanunue kwa bei wanayotaka isiyozidi 800/=. Pamoja na uvumilivu wote ulioonyeshwa na wakulima wa Pamba nchini kwa miaka yote hiyo 49 bado Serikali haiwajali. Baadhi ya wabunge walilazimika kuomba mwongozo wa Spika ili kumchukulia hatua Waziri Mkuu kwa UBABAISHAJI.
My take:
1. Serikali ya Magamba imeona ishushe bei ili kuwakomoa wakulima wa Pamba kwa sababu karibu majimbo mengi ya uchaguzi yanayolima Pamba wabunge wake ni wa UPINZANI.
2. Waliwalainisha ili wapate KURA lakini wananchi wamewashitukia na Serikali nayo imekengeuka.
3. Ni mtindo wa Serikali kununua Pamba kwa bei ndogo ili wapate pamba ya kutosha ya kutengeneza T-shirt, Kofia na Kanga za Magamba kwa ajili ya kuzigawa bure wakati wa uchaguzi.