BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
BULGARIA: Wakulima wakubwa na Wadogo wameandamana kwa siku ya pili walishinikiza Serikali kuweka Uongozi Unaowajibika pamoja na kuongezwa kwa Fedha za Ruzuku ya Kilimo nchini humo.
Kamati ya Mipango ya Wakulima hao imesema Umoja huo hautasitisha Maandamano hayo hadi Waziri wa Kilimo, Kiril Videev atakapojiuzulu huku wakitishia kufunga maeneo muhimu ya kuingia Mjini ikiwemo kumwaga maelfu ya Lita za Maziwa Barabarani.
Pia, Wakulima hao wamedai kuwa endapo Serikali ikipuuza matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuzuia uagizwaji wa Ngano kutoka Ukraine, kuanzia Wiki ijayo wataingiza Mifugo wakiwemo Ng'ombe katikati ya Majiji yote.
=========