Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We unafikiri manyanyaso yameanza jana,au yataanza hao mabepari wakianza kulima?Habari wna bodi
Wiki iliyopita nilikua na ziara yangu binafsi katika baadhi ya vijiji vya mkoa wa Iringa. Nimejionea mashamba makubwa ya mahindi yanamwagiliwa kwa mitambo. Kwa sasa wenyeji wanasubiri mvua ndo walime wale wawekezaji mahindi yao yaanaanza kuchanua. Kwa hali hii ikiendelea miaka mitatu ijayo tutakua na haya
1. wakulima wadogo wote watageuka vibarua kwenye mashamba ya hawa mabepari maana hawatakua na uwezo wa kulima katika mashamba yao kutokana na bei kubwa hizi za mbolea
2. Hakutakua na mkulima mdogo bali wote tutategemea kununua unga kutoka kwa hawa mabepari wenye mashamba makubwa
3. Tutakua tunafanya vibarua kwenye haya mashamba kwa kunyanyaswa na kipato kidogo tutakachopata kitaishia kununua chakula( Tunageuka watumwa kwenye ardhi zetu)