Nakumbuka nilipigana darasani na mshkaji mmoja alikuaga kipanga wa darasa yule jamaa alikua anapendwa na walimu balaa na kila tukifunga shule yeye alikua anaondoka na zawadi namba 1 kuanzia la kwanza mpaka la Saba ni namba 1 hata tukienda kufanya mitihani na shule jirani kipindi kile jamaa alikua anawakalisha shule yetu inaongoza, alipomaliza la Saba kipindi kile ilikua ngumu kuingia shule za Serikali sekondari wengine walikua hadi wanahonga kukwepa kupeleka watoto wao private gharama, jamaa akapelekwa shule nzuri tu ya private ipo maeneo ya Mbagara (nadhani walishauri walimu shule ya msingi X) alipoenda pale private yeye ni kuwanyoosha mwanzo mwisho, kutokana na ufaulu wake kua mkubwa akapewa nafasi special awe anasoma bure yaan yeye MALIPO yake ni kusoma na kufanya vizuri tu gharama zingine zote shule itamlipia, ukiangalia jamaa kwao wote wamesoma bure sababu wana akili, yeye, dada yake na kaka yake, yeye alisoma bure mpaka advance shule binafsi akalipiwa kila kitu na alipomaliza pia akapata connection ya kazi bank moja ya biashara Mjini Dasalama kabla hajaenda Chuo, hii ni kwa wachache Sana japokua advance alisoma ECA na sijui walitumia utaratibu gani
Ilikua hivi siku ya tukio nikiwa nasoma shule ya msingi X maeneo ya Ubungo nikiwa kijana mdogo sana nisiezidi miaka 9 kuna zile karamu za risasi tulikua tunachorea chorea kwenye somo la stadi za kazi, historia & Maarifa ya Jamii, sasa Mimi na yeye siku hio sijui ilikua kuaje tukawa tumekaa karibu nikawa nimeazima karamu ya risasi bahati mbaya kwenye kuchora ile karamu yake ikakatika nilishtukia tu nimekula banzi la kichwa, na jamΓ a japo kua alikua ni kipanga wa darasa Ila pia alikua jamΓ a muonevu sana na mwishoni kabisa alikuja kua kitombi hatari pindi tunafika darasa la 6 kwenda la 7 yaan jamΓ a alikua anapenda sana sana story story za ngono ngono story za Malaya na Makahaba alikua anazijua ukiangalia umri wake hauzidi miaka 15 Ila ndio kichwa balaa HESABU kwake ni km maji anazikata hakosei hata kidogo
Basi kipindi kile hio shule msingi X ya Serikali maeneo ya Ubungo ilikua na dawati za chuma dawati za mbao zilikua chache tena zililetwa kwa msaada wa NMB yaan madarasa mengi Ila madawati machache, unaambiwa tulipigana rushana sana kwenye machuma jamaa alipoona namzidi nguvu maana Mimi nilikua mrefu nimepanda hewani yeye ni mfupi akatumia makucha mΓ ana alikua anafuga makucha akanikwarua usoni nikasema isiwe tabu wewe mweupe Mimi mweusi leo utakua mwekundu nimbilingisha yeye akawa Chini Mimi nipo juu nimemkalia tumboni nikakunja ngumi haswaa nikamlenga ngumi kadhaa za usoni huku nikimtoa mikono ili ngumu zimuingie usoni piga usoni nikaona damu unaanza kumtoka puani piga ngumi nyingi hadi jamaa wakaja kutuamua
Ugomvi ukazimwa chini chini hata walimu waliposikia anaepigana ni kipanga mmoja na mtulivu mmoja wa darasa hana baya na mtu na hawana record zake zozote mbaya za kinidhamu wakasema hao acha wamalizane wenyewe basi, inavyokua masuala ya shule za msingi na masuala ya utoto hua kunakuaga na kitu kinaitwa rematch yaan pambano hili lirudiwe na kurudiwa linaenda kurudiwa jioni baada ya kutoka shule kwenye uwanja wa mapambano nje kidogo ya shule na huo mchezo ulikuepo shule nzima yaan watu wakipigana tu ndani maana shule imezungushiwa ukuta mkubwa wasipotosheka ndani ya shule darasani hajapatikana mshindi basi inaandaliwa rematch jioni mkitoka team 2 zinakutana uwanjani ngumi zinaenda kupigwa tena upya mpaka mtu atoke damu, alie, atubu, aombe msamaha na mshindi apatikane, yaan inapigwa ngumi kweli kweli na damu unamwagika kweli wanafunzi wana vituko sana
Jamaa zake walipomwangalia jamaa kaiva sura nyekundu wakasema rematch Jioni tunaenda uwanjani nikasema sawa Mimi yule namweza na kule uwanjani ntamtoa meno kabisa na atatubu ataomba poo, kumbuka hapo Mimi sina wapambe yaan team yangu nipo peke yangu Mimi km Mimi tu na yeye team yake ni kikosi wapo wengi almost darasa zima wapo upande wake na madarasa ya jirani wameungana nae
Basi jioni baada ya vipindi kuna jamaa mmoja yeye alikua kiranja rafiki yangu Sana tulikua tunasoma pamoja tuition na hatukai mbali yaan unapita kwao ndio unaenda kwetu akanifuata hapo nishatoka getini naelekea uwanjani mdogo mdogo nikazipange paringi mtu bee yaan nawaza ntakavyomtwanga km Bruce Lee alafu wao walikua mbele wametangulia Mimi nakuja nyuma peke yangu, jamaa kiranja akanifuata akaniambia sikia wale jamΓ a hawana nia njema na wewe wanaenda kukuchangia wote watakuumiza huko uwanjani hicho ndicho walichokipanga kwa hio usiende watakuumiza hata Mimi nilikuepo wakati wanapanga hio njama nimesikia yote wamesema usiende wataenda kukuumiza
Nikimwangalia jamaa hajawahi niambia uongo na nikiangalia lile kundi ndio wanichangie wapo zaidi ya 50 hata km kweli nilikua na mafunzo ya Judo, Karate, Tai Kwando na Tai Chi kwa kipindi kile siwezi nikapukutisha watu zaidi ya 50 wanaonichangia kwa pamoja wangeniua pale uwanjani
Nikasema sawa isiwe tabu kwenye ile njia ya barabara inayoelekea uwanjani kulikua kuna sehemu kuna chochoro alafu mbele kidogo kuna njiapanda njia moja inaenda uwanjani na nyingine inaenda barabarani nikafika pale njiapanda nikaona isiwe tabu yanini kwenda kufa nikanyoosha ya barabara mpaka stand tafuta Gari ya home huyooo mpaka home uwanjani sikwenda kupigana walinisubiri hadi wakaamua kuondoka