Mjendi
Member
- Mar 28, 2020
- 88
- 102
#Kelv
Magufuli kuwanyima wapinzani wake kufanya siasa kwa miaka mitano iliyopita ni kosa kubwa sana la kimkakati amelifanya na atalijutia hili kwa maisha yake yote.
Yeye tayari ameshawakinai watu na sera zake za kibabe na sasa watu wana shauku kubwa na Lissu ambaye hawajamsikia kabisa.
Halafu ccm lazima wakubali hili wapende wasipende, kumshambulia Lissu kwa nia ya kutaka kumuua nalo ni kosa kubwa sana walilotenda na madhara yake watakuja kuyaona kwenye uchaguzi.
Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM ilihitaji uwepo wa Mzee Mkapa kuliko kipindi kingine chochote kile, labda ukiondoa wakati ule wa mchakato wa kumpata Rais wa awamu ya tano.
Hesabu hazisomi vizuri kabisa, angalau ule waraka wa wastaafu ungetumika kuiweka timu pamoja badala ya kudukua faragha zao na kuwaadhibu hadharani na mwanaharakati huru MUSIBA ameahidi kula sahani moja na Wapinzani kosa lingne la kimkakati hili wanalitengeneza Watawala!
Polepole na Bashiru wangetosha sana kukisemea chama na Gerson angetosha kumsemea Magufuli pale Ikulu! Yaani mzee asingepaniki namna ile pale Dodoma!
Sasa Wote wanawashwa Mkuu anawashwa...Polepole anawashwa...Gerson anawashwa...Mkunaji ni Mpinzani mkunwaji ni Mtawala!
Tukutane Oktoba.....kwa wenye Upele wakunaji wameshafuga kucha kwa hiyo Upele wenu kwao ni kwele!
By
Kelvin hk