Wakunyumba tradional party; sasa siku zinahesabika

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Ile sherehe kubwa, ile dhifa ya kiasili, ile pati ya aina yake, ile shughuli ya ukweli, inayojulikana kwa jina la Wakunyumba Tradional Party itakayowakutanisha Watanzania kutoka Kabila la Wangoni, sasa siku za tukio zinahesibika.

Bado siku 27 tu! Kuifikia siku ya tarehe 14, Agossti 2026, Ijumaa ya saa 10 jioni ambapo ukumbi maarufu uliyopo katika Jengo la Makumbusho ya Taifa (Tanzania National Museum) lililopo maeneo ya Posta Mpya jijini Dar utakapong'arishwa na pati hiyo.

Unakosaje sasa? Kwa sababu, mamodo, masupa staa wa Bongo, viongozi maarufu wa kisiasa na kijamii nchini na wananchi kutoka Kabila la Wangoni, watakuwepo.

Watu wa kutoka makabila wengine pia watakuwepo kuungana na Wangoni katika kudumisha ushirikiano.

Pati hiyo iliyoandaliwa na Mwendo wa Saa Production (Ngoni By DNA), ina lengo la kukumbusha mila, tamaduni na desturi za Kabila la Wangoni huku historia ya kabila hilo ikisimuliwa kuanzia lilikotokea, lilikopita hadi liko sasa ambapo ni mjini Songea, mkoani Ruvuma.

Sherehe hii itakuwa endelevu kwa sababu itakuwa ikifanyika kila mwaka katika ukumbi au eneo litakalochaguliwa na kamati ya maandalizi ya Mwendo wa Saa Production.

Watu wote wanakaribishwa kuhudhuria siku hiyo kwa sababu itakuwa siku ya kipekee na kuvutia mno.
Rangi nzuri ya kijani iliyoiva na mapambo ya asili ya jamii ya Wangoni yenye kitambaa chenye mwonekano wa mnyama Chui (chuichui) na ngozi na magome ya miti ya migomba vitapamba mwonekano wa sehemu yote ya shughuli.

Aidha, siku hiyohiyo itakayobeba kumbukumbu ya maisha ya wahudhuriaji, kutakuwa na vyakula vya asili ya Wangoni; kama vile nyama choma (zitazochomwa kwenye grill) na ugali wa unga wa ulezi, mtama na mahindi.
Pia kutakuwa na kachumbari iliyoandaliwa vizuri na mboga za majani, ikiwemo mboga maarufu ya Wangoni iitwayo 'likolo la nanyungu' (majani ya maboga).

Wageni wakiwa wanaongea kwa furaha ya tukio, watainjoi kusikiliza muziki (wa back ground) ambao nao ni nyimbo za Kingoni zinazofahamika.

Kutakuwa na vinywaji vya aina nyingi mchanganyiko. Vyenye kilevi, vinywaji laini, coctail na maji. Pia kutakuwa na pombe za asili; kama vile kangara, mnazi, mtama n.k.

Wasanii wa nyimbo za jamii ya Wangoni wataimba kwaya na kucheza ngoma mbalimbali za Kingoni zikiwemo Kitoto, Ligwamba, Lizombe, Beta n.k.

Waandaaji watatoa Tuzo kwa msanii Mngoni aliyedumisha/anayedumisha mila, desturi na tamaduni za Wangoni mpaka zama hizi.

Kiingilio cha siku hiyo ya mtoko mzuri ni Shilingi 50,000 (kwa ngazi ya kawaida) Shilingi 100,000 (kwa V.I.P) na Shilingi 200,000 (kwa V.V.I.P).

Utamaduni wetu; Tuukumbuke, Tuuheshimu, Tujivunie.

Unakosaje kufika sasa? Nyumbi hii...Bombi hii.

Imeandaliwa na: Lucy F. Komba, Mkurugenzi Mtendaji wa MS PRODUCTION.


​
 
Bila kucheza kioda, mganda na ile ngoma ya kukatika siji
 
Nyie kina ngongi mwendo WA saa naona mnarudi kivingine. Hongereni sana
 
Ati mkipewa hela zinafika, ila mwanamke umwelekeze huyo hafiki, kweli?
 
Jitahidini wale Ngoni Tribe walioimba Madungayembe wawepo, "wanawake wazuri wazuri wameolewa,yamebaki madungayembe yanahangaika"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…