Wakunyumba traditional party; Dk. Emmanuel nchini atarajiwa ugeni rasmi wa hafla

Wakunyumba traditional party; Dk. Emmanuel nchini atarajiwa ugeni rasmi wa hafla

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Zikiwa zimesalia siku 27 kuifikia Agosti 14, 2026 ili kufanyika hafla kubwa ya Wangoni Traditional Party, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dk. Emmauel John Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa tukio hilo la kipekee.

Hafla hiyo inayowakutanisha jamii ya watu kutoka kabila maarufu la Wangoni, itafanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliyopo maeneo ya Posta Mpya, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa muandaaji wa hafla hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MS Production, Lucy Francis Komba, tayari wapo katika mazungumzo ya kiofisi ili kumpata Makamu wa Rais kuwa mgeni rasmi. Kwa hiyo, mambo yakikamilika, jamii itajulishwa rasmi.

"Wakunyumba Traditional Party ipo karibu sana. Bado kama siku ishirini na saba tu kufikia siku ya tukio. Ni Agosti 14 mwaka huu. Pale Makumbusho ya Taifa.

"Hadi sasa tunapambana kiofisi ili tumpate mgeni rasmi ambaye tumeona Makamu wa Rais, Balozi Emmanuel Nchimbi ndiyo anastahili. Tuko katika mawasiliano," alisema Lucy Komba.

Aidha, Lucy alisisitiza kuwa, mbali na kufanya mawasiliano ya kiofisi ili kumpata Balozi Nchimbi, pia idadi kubwa ya mastaa wa Bongo ambao ni kutoka kabila la Wangoni wanatarajiwa kushiriki.
"Pia kuna mastaa wakubwa ambao wanatoka Kabila la Wangoni tunatarajia watashiriki. Kama mjuavyo, Kabila la Wangoni linatoa watu wengi maarufu hapa nchini," alisema Lucy.

Aliwataja baadhi ya masupastaa hao ambao wanatarajiwa kuwepo ni; Jokate Urban Mwegelo ambaye ni Katibu Mkuu Mstaafu wa UV-CCM, Shamila Ndangwila (Bi. Star) ambaye kwa sasa anavuma sana kwa jina la Mwadawa kupitia Tamthiliya ya Kombolelo.

Aidha, kuna Angel John Komba (Winter) ambaye anawika kwa sasa kwa jina la Tukae kupitia Thamthiliya la Kombolela na Walter Chilambo, Mshindi wa Bongo Star Search (BSS) mwaka 2015 ambaye pia atatarajiwa kuwepo.

Wengine ni; Joseph Leonard Haule maarufu kama Peofesa Jey ambaye ni nguli wa Muziki wa Bongo Fleva na mbunge mstaafu wa Jimbo la Mikumi na Cosmas Thobias Chidumule mwanamuziki mstaafu wa Bendi ya DDC Mlimani Park na mwimbaji wa Nyimbo za Injili kwa sasa akitamba na wimbo wake wa Yesu ni Bwana.

Lucy, aliwataja wengine wanaotarajiwa kuwepo kuwa ni Joseph Osmundi Mbilinyi 'Sugu', ambaye ni mkongwe na mwanzilishi wa muziki wa Bongo Fleva, Mrisho Mpoto 'Mjomba' ambaye ni mghani wa nyimbo za mashairi Bongo na Rose Donatus Ndauka, nyota wa sinema za Bongo.

"Sijamaliza. Wengine ambao tunatarajia wawepo ni Dickson Samson Makwaya (Bambo) (muigizaji/mchekeshaji), Lulu Mapunda (Aunt Lulu) (mwigizaji), Jacqueline Nachale (Jack Mngoni) (mchekeshaji), Mkono wa Mkonole (muigizaji na mchekeshaji), Producer Mr. T na Producer C9 Kanjenje," alisema Lucy Komba.
Screenshot_20260728_204118_Google.jpg
 
Kwa hiyo ima atakuja kucheza Ngoma kidogo
 
Back
Top Bottom