BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakurugenzi na Maafisa 6 wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) wamesimamishwa kazi kwa muda kuanzia Aprili 3, 2024 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.
Baadhi ya tuhuma hizo ni pamoja na kukiuka taratibu na kanuni za uendeshaji wa Mashirika ya Umma
Waliopumzishwa ni
1. CPA Savo Mung'ong'o (Mkurugenzi wa Fedha na Masoko)
2. Mhandisi Victor Kamagenge (Mkurugenzi wa Miliki na Miradi)
3. Mkunde Mushi (Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko)
4. Festo Mramba (Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu na Utawala)
5. CPA Augustine Karadoga (Mhasibu Mkuu)
6. Catherine Kilinda (Meneja JNICC)
Taarifa ya AICC imesema taratibu nyingine za Kisheria zilizochukuliwa zitatangazwa baadaye.