DOKEZO Wakurugenzi na Wakuu wa Idara (sana sana DMO's na DEO's) wamekuwa kikwazo kwenye zoezi zima la uhamisho wa watumishi kwa mfumo mpya ESS

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Na hapo mtumishi akihama bado kuhamishiwa mshahara napo ni usumbufu mwingine. Mtu anahama mwezi wa 4 mpaka mwezi huu october bado mshahara haujahamishwa. Kichekesho utumishi anakujibu kuwa mfumo umebadilika na hakwenda kwenye semina hivyo hajui kuhamisha. Sasa najiuliza kwenye hizo ofisi wanafanya nini..? Si waondolewe watu wanaotafuta ajira ni wengi sana kwa sasa zaidi ya hao wanaofanya mambo hovyo hovyo
 
Sure
 
Huu mtindo ni uhuni kuna watu wamahamishwa tena kwa kuanza mwaka ya fedha ila mshahara wao haujahama ,yaani mtu amehamishwa mwezi wa 7 na kuripot mwezi wa 8 ila bado wanasema mpaka check number ifanyiwe vetting na kupelekwa taasisi mpya ....

Mpaka mwaka unageuka yaani mwezi wa kwanza bado na ukipiga hesabu mwezi wa saba mpaka wa kwanza ni miezi kama 5 ila wanasumbuka ni hovyo kabisa.

Wengine stahiki zao bado eti wanakaa vikao vya nn tena!? Sheria zipo wazi mtu apewe chake.
 
Sana mkuu kupitia andiko hili naanza kuelewa kwann hawahamishi mishahara kwa wakati. Ili wapate kaujanja kaa kwenda semina za posho mara kwa mara
 
Sana mkuu kupitia andiko hili naanza kuelewa kwann hawahamishi mishahara kwa wakati. Ili wapate kaujanja kaa kwenda semina za posho mara kwa mara
Mwaka 2019 tuliomba stahiki zetu ,HR anasema mpaka wakae vikao na mda huo sisi tusharipot vituoni huoni kama kuna ujinga sana hapo!?
 
Mwaka 2019 tuliomba stahiki zetu ,HR anasema mpaka wakae vikao na mda huo sisi tusharipot vituoni huoni kama kuna ujinga sana hapo!?
Sana mkuu ajira za afya na elimu mwaka huu toka 07/2023 mpaka now 10/2023 bado wapo ambao hawajawekewa hela za kujikimu
 
Yes ndani ya Mkoa pia ila changamoto iko pale pale Ma supervisor wa Mfumo wanasema hawana elimu na mfumo [emoji1787][emoji1787]

Namaanisha kutoka kituo kimoja kwenda kingine ndan ya halmshauri
 
Ningestuka kama nisingeona Halmashauri za kigoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…