DOKEZO Wakurugenzi na Wakuu wa Idara (sana sana DMO's na DEO's) wamekuwa kikwazo kwenye zoezi zima la uhamisho wa watumishi kwa mfumo mpya ESS

DOKEZO Wakurugenzi na Wakuu wa Idara (sana sana DMO's na DEO's) wamekuwa kikwazo kwenye zoezi zima la uhamisho wa watumishi kwa mfumo mpya ESS

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna mgomo baridi labda..

Maana nasikia Semina walienda DHROs/Wakkuu wa idara ya Utumishi.

Wanaofanya kazi ni Maafisa Utumishi, kwahiyo wanajifanya hawaelei kitu.
Maafisa utumishi nao wanataka rushwa nimetonywa hiyo na jamaa wa ofisi
 
Habari zenu wakuu
Shida huu mfumo ukitaka kukopa pia ni changamoto una errors nyingi na sana
 
Habari zenu wakuu
Shida huu mfumo ukitaka kukopa pia ni changamoto una errors nyingi na sana
Try as much as possible ni system tu inacheza,andaa pia hela ya kumuhonga HRO ili mambo yaende haraka maana utumishi hawana taarifa kama bado unafanya kazi au umeshaacha

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
mtu anayeweza kunisadia Mke wangu akahama aisee nitampa pesa, sina namna, nilishatoa pesa mara ya kwanza ikaliwa ila sijachoka
 
Mimi nilifanya Transfer Vacancy Request kwenda taasisi nyingine wakaiReject, na wakatoa sababu ya kureject.

Sasa kila nikijaribu kuomba sehemu nyingine wananiandikia "YOU HAVE OTHER PENDING REQUEST" ambayo tayari walishaiReject.

Nashindwa kwenda mbele, nashindwa kurudi nyuma. Na option ya kuiDelete ile request iliyokataliwa hamna.

Msaada wanakwetu wenye kujua jinsi ya kichomoka hapo.
 
Delete Ile transfer ya mwanzo
 
WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA (SANA SANA DMO's na DEO's) WAMEKUWA KIKWAZO KWENYE ZOEZI ZIMA LA UHAMISHO WA WATUMISHI KWA KISINGIZIO CHA KUTOKUWA ORIENTED NA MFUMO MPYA WA HUDUMA YA UHAMISHO WA WATUMISHI ESS

Habari za Asubuhi wanajamvi,

Nimeleta habari hii baada ya kujiridhisha na kufanya Tafiti mbalimbali kugundua kama walichoniambia wadau hao ni kweli au lah na baada ya kugundua ukweli nimekuja na mada hii.

Itakumbukwa kwamba Rasmi Serikali kupitia wizara ya OR-Utumishi ilisitisha Katibu mkuu Tamisemi na KATIBU MKUU Utumishi kupokea maombi ya uhamisho Wa barua na kuanzisha mfumo wa uhamisho serkalini wenye Taarifa za mtumishi kupitia ess.utumishi.go.tz.

Kwa kuona kwamba uhamisho kwa njia ya zamani ilikuwa inapoteza Mudabwa mtumisho ,Haukusa rafiki kwa mtumishi na Kuongeza njia za ushawishi wa rushwa kwa Pande hizo mbili.

hivyo kwa maelekezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais–Utumishi aliyoyatoa kupitia barua yenye Kumb Na. FA.228/613/01/1 ya tarehe 11 Agosti, 2023. Kuhusu Mfumo huo.

TATIZO LILIPOANZA...

Baada ya barua hiyo Wakuu wa Idara na MaDED walikataa barua zote zilizokuja Kwao kuanzia Tarehe 01/09/2023 kwa kisingizio cha wamepewa maelekezo kuwa mtumishi aombe uhamisho kupitia Mfumo wa kiutumishi wa uhamisho.

Baadhi ya watumishi kwa kuwa wanajua Technolojia waliomba na matokeo yake waliporudi kwa maafiaa utumishi na waajiri na WAKUU wa idara zao ili waaprove kulitoa ombi kwa supervisor waliwajibu kwamba hawajui chochote kuhusu mfumo hivyo hawatafanya lolote.

Sasa Kama wamekataa paperwork na mfumo bado hawaufahamu.

Je, hii ni Njia mpya ya serikali kuzuia uhamisho kwa Watumishi?

Na kama sio serikali Imechukua jukumu Gani kuhakikisha mfumi unafanya kazi tena kwa Ufanisi na kwa muda?

Sehemu mpaka Sasa zinazolalamikiwa ambzo nimefanya Reseach huko Halmashauri ya wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya wilaya ya kwimba, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya manispaa ya Ubungo, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.

Halmashauri ya wilaya ya Muheza, Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Halmashauri ya wilaya ya Pangani, Halmashauri ya manispaa ya singida, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe ,Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.

hizi ni baadhi tu na ndo zenye malalamiko mengi ila yapo halmashauri za majiji na manispaa ambazo zima malalamiko machache.

SERIKALI KAMA MMEAMUA KUZUIA UHAMISHO KWA WATUMISHI MSILETE VISINGIZIO MAANA MAJIBU MENGI YA WAKURUGENZI NI KUWA TUNAFATA MAELEKEZO.

Sasa mtumishi afanye lipi mmemzuia Kufanya uhamisho wa barua na bado baadhi ya Waajiri wanazuia uhamisho wa Mtandao.
Hatar kwel😭
 
Mimi nilifanya Transfer Vacancy Request kwenda taasisi nyingine wakaiReject, na wakatoa sababu ya kureject.

Sasa kila nikijaribu kuomba sehemu nyingine wananiandikia "YOU HAVE OTHER PENDING REQUEST" ambayo tayari walishaiReject.

Nashindwa kwenda mbele, nashindwa kurudi nyuma. Na option ya kuiDelete ile request iliyokataliwa hamna.

Msaada wanakwetu wenye kujua jinsi ya kichomoka hapo.
Nini tofauti ya TRANSFER REQUEST NA VACANCY REQUEST?
 
Back
Top Bottom