Wakurugenzi wa halmashauri watii agizo la Rais Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais Magufuli alitoa agizo la kuwataka DEDs wa halmashauri zilizo vijijini lakini wenyewe wanaishi mjini kuhamia maeneo yao ya kazi ndani ya siku 30 na mwisho ni tarehe 07/11/2019.

DED wa Tarime vijijini ameshafungasha virago na tayari yuko kijijini na amewataka watumishi wote kuwa wamehamia kufikia tarehe hiyo ya mwisho.

Naye RC Chalamila wa Mbeya amempa Ded wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya masaa 24 kuondoka jijini humo yeye na watumishi wake na kuwafuata wananchi kijijini.

Chalamila amesema ameandaa gari la jeshi, gari la polisi na gari la magereza kwa ajili ya kubeba nyaraka za serikali katika uhamisho huo.

Chanzo: TBC
 
Hii ya Mbeya ni safi sana. Nilikuwa nashangaa sana inakuwaje halmashauri ya Mbeya vijijini ipo katikati ya mji wa mbeya karibu kabisa na halmashauri ya jiji la Mbeya. Kama itaendelea kuwa hivyo, hakuna maana ya kuwa na halmashauri hiyo. Tutakuwa hatujapeleka huduma karibu na wananchi. Sijui watakuwa wameelekea wapi?
 
Hii tabia ilikuwa imeita mizizi ,siku fulani kabla ya rais kutoa agizo hilo tulikuwa kwenye ukaguzi wa miradi ya barabara inayowahusu sumbawanga vijijini sasa nikiwa kwenye gari nikatoa hoja kwamba inakuaje sumbawanga DC wako mjini wakati inahudumia vijijini? Nikawaambia ilifaa wahamie Laela ili kusogeza huduma kwa wananchi na kutoa fursa ya mji wa Laela kukua
Basi wakani crash wee,kama niliota vile punde Rais alipokuja akatoa agizo kama nilivyokuwa nawaza,nikaishia kuwacheka huko whatsup baada ya kuumbuka.Nashukuru Rais ameifanya kuwa amri ya nchi nzima na halmashauri 31 zinahusika
 
Mbeya vijijini wataelekea wapi Mkuu? Iwalanje? Igawilo? Nsalaga? Songwe au wapi?
 
Hii ya Mbeya ni safi sana. Nilikuwa nashangaa sana inakuwaje halmashauri ya Mbeya vijijini ipo katikati ya mji wa mbeya karibu kabisa na halmashauri ya jiji la Mbeya. Kama itaendelea kuwa hivyo, hakuna maana ya kuwa na halmashauri hiyo. Tutakuwa hatujapeleka huduma karibu na wananchi. Sijui watakuwa wameelekea wapi?
Wanahamia mbalizi unamlazimishaje mtumishi akakae mbalizi ilihali nyumba Yake ipo iwambi
 
Hii ya Mbeya ni safi sana. Nilikuwa nashangaa sana inakuwaje halmashauri ya Mbeya vijijini ipo katikati ya mji wa mbeya karibu kabisa na halmashauri ya jiji la Mbeya. Kama itaendelea kuwa hivyo, hakuna maana ya kuwa na halmashauri hiyo. Tutakuwa hatujapeleka huduma karibu na wananchi. Sijui watakuwa wameelekea wapi?
Saa hizi watakuwa wanahamisha samani za ofisini!
 
Hii tabia ilikuwa imeita mizizi ,siku fulani kabla ya rais kutoa agizo hilo tulikuwa kwenye ukaguzi wa miradi ya barabara inayowahusu sumbawanga vijijini sasa nikiwa kwenye gari nikatoa hoja kwamba inakuaje sumbawanga DC wako mjini wakati inahudumia vijijini? Nikawaambia ilifaa wahamie Laela ili kusogeza huduma kwa wananchi na kutoa fursa ya mji wa Laela kukua
Basi wakani crash wee,kama niliota vile punde Rais alipokuja akatoa agizo kama nilivyokuwa nawaza,nikaishia kuwacheka huko whatsup baada ya kuumbuka.Nashukuru Rais ameifanya kuwa amri ya nchi nzima na halmashauri 31 zinahusika
Lindi vijijini inahamia Mtama na Iringa vijijini inahamia Kalenga!
 
mkuu kwa jinsi wilaya ya mbeya vijijini ilivyo kigeographia sijui watahamia wapi!!!...... wakihamia mbalizi imagine mtu wa igoma &ifupa atahudumiwa vp?...... yan hii wilaya waliigawa kipumbavu kabisa
Hii ya Mbeya ni safi sana. Nilikuwa nashangaa sana inakuwaje halmashauri ya Mbeya vijijini ipo katikati ya mji wa mbeya karibu kabisa na halmashauri ya jiji la Mbeya. Kama itaendelea kuwa hivyo, hakuna maana ya kuwa na halmashauri hiyo. Tutakuwa hatujapeleka huduma karibu na wananchi. Sijui watakuwa wameelekea wapi?
 
mkuu kwa jinsi wilaya ya mbeya vijijini ilivyo kigeographia sijui watahamia wapi!!!...... wakihamia mbalizi imagine mtu wa igoma &ifupa atahudumiwa vp?...... yan hii wilaya waliigawa kipumbavu kabisa
Mkoa wa Pwani ndio Funga Kazi makao makuu ya mkoa yako kibaha mtu wa wilaya ya rufiji au mkuranga akitaka kwenda makao makuu ya mkoa lazima apitie mkoa wa dar es salaam aumalize ndipo afike makao makuu ya mkoa wake
 
Kuwahamishia hao maafisa huko vijijini ni sawasawa na uamuzi wa kuhamia Dodoma ulivyokuwa unasuasua. Ni vema logistics na utashi utumike ikiwemo mijadala ya kuamua ni eneo gani muafaka zaidi kupunguza uwezekanao wa watu kuwa wanasafiri kila mara kurudi mjini kupata mahitaji na huduma. Napendekeza kama logistics hazijakaa vizuri sana, wale maafisa ambao kwa nature ya kazi zao wanatakiwa wawe karibu kabisa na maeneo yao ya kazi, mfano maafisa ugani wanaweza wakahamia huko huku wakipewa nyumba na vitendea kazi kama pikipiki kabla ya kuwahamisha maafisa wengine kama mkurugenzi na wakuu wa idara, DC na maofisa wake nk.
 
mkuu kwa jinsi wilaya ya mbeya vijijini ilivyo kigeographia sijui watahamia wapi!!!...... wakihamia mbalizi imagine mtu wa igoma &ifupa atahudumiwa vp?...... yan hii wilaya waliigawa kipumbavu kabisa
Igoma ni jirani sana,nyingi ya halmashauri za vijijini huwa zinazunguka jiji au mji sasa kiuhalisia huwa kunakuwa na changamoto kidogo kwa baadhi ya maeneo kuwa mbali sana
 
Back
Top Bottom