Kuwahamishia hao maafisa huko vijijini ni sawasawa na uamuzi wa kuhamia Dodoma ulivyokuwa unasuasua. Ni vema logistics na utashi utumike ikiwemo mijadala ya kuamua ni eneo gani muafaka zaidi kupunguza uwezekanao wa watu kuwa wanasafiri kila mara kurudi mjini kupata mahitaji na huduma. Napendekeza kama logistics hazijakaa vizuri sana, wale maafisa ambao kwa nature ya kazi zao wanatakiwa wawe karibu kabisa na maeneo yao ya kazi, mfano maafisa ugani wanaweza wakahamia huko huku wakipewa nyumba na vitendea kazi kama pikipiki kabla ya kuwahamisha maafisa wengine kama mkurugenzi na wakuu wa idara, DC na maofisa wake nk.