Wakurugenzi wa halmashauri watii agizo la Rais Magufuli

DC hawezi halazimiki kuhamia kijijini kwa sababu anahudumia halmashauri mbili mfano DC wa Mbeya anasimamia halmashauri ya Mbeya vijijini na Mbeya jiji hapo ahamie kijijini kufanyaje?
 
Hili jambo siyo la kufurahia bila tafakari. Tatizo la watendaji wa halmashauri kuishi katikati ya mji limekuwa zaidi kwa zile halmashauri ambazo maeneo yake ya kiutawala yanauzunguka mji/jiji.

Ofisi za halmashauri hizo zilikuwa kwenye mji au jiji kwa sababu hapo ni kama katikati ya maeneo yote yanayouzunguka mji au jiji. Sasa wanapoondolewa hapo ni lazima wataelekea upande mmojawapo na kuwafanya kuwa mbali zaidi na maeneo yao ya kiutawala kwa baadhi ya maeneo.
 
Nasikia Madiwani na Watumishi waandamizi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi wanapanga kubadili gia angani kwa kutaka kuihamishia Halmashauri kwa wauza mafuta ya dili wa Nyololo, badala ya Igowole kulikostahili kujengwa na ndiko kuliko idhinishwa na hilo Baraza la Madiwani na pia Mkuu wa Mkoa wa Iringa wa wakati huo (Amina Masenza)

Nasikia sababu ni mvutano wa kimaendeleo! Kila diwani anavutia kwake, na sababu nyingine ni kutaka tu kuwa jirani na makazi yao yaliyoko Mafinga. Sasa unajiuliza hapo Nyololo hakuna chochote cha maana zaidi tu ya kuwa kando ya barabara kuu ya TanZam.

Nadhani Waziri Jaffo anatakiwa awatembelee tena hao waheshimiwa.
 
Naunga mkono Nyololo!

Kasesela walitaka kumpeleka Isimani......akawaambia Kalenga panatosha!
 
Mkoa wa Pwani ndio Funga Kazi makao makuu ya mkoa yako kibaha mtu wa wilaya ya rufiji au mkuranga akitaka kwenda makao makuu ya mkoa lazima apitie mkoa wa dar es salaam aumalize ndipo afike makao makuu ya mkoa wake
Unashauri yawekwe wapi?
 

..kwanini tumetumia fedha nyingi kuhamia DODOMA, wakati kuna wilaya kibao watumishi wake hawana ofisi na makazi?
 
Bukoba vijijini imekaaje pale Rwamishenye? Kemondo mji unajiozea na bandari yake.
 
Hata shinyanga pia, halmasahuri ya shinyanga mjini na shinyanga mjini zinatenganishwa na barabara tu.
 
Mkifikilia kwa haraka utaona ni maamuzi sahihi, ila ukienda kwa kina sana yana madhara makubwa sana.
 
Wacha ubaguzi........Mkurugenzi na timu yake wawe wa kwanza kuhamia vijijini
 
inashangaza sana suala kama hili kusubiri agizo la Mheshimiwa Rais. Ama hakika Urais kwa Nchi hii ni kazi ngumu sana. Watendaji wengi wanakosa creativity na kusubiri maagizo tu!
 
Hivi wale bado wanamsema vibaya Magufuli wana nia gani kweli, huyu ndiye rais wa wanyonge, huduma za kiserikali sasa zinakaribia watu vijijini, umeme pia vijijini, watu wataanza kurudi kwao mikoani na kuwekeza vijijini, hamna haja ya kusongamana mijini.
 
Hawajajenga ofisi yao?
 
Mbeya vijijini wataelekea wapi Mkuu? Iwalanje? Igawilo? Nsalaga? Songwe au wapi?
Tupo Inyala hapa..Tumepania kuwatumikia wananchi kwa moyo wa upendo na hata wananchi wasilslamike kuhusu wake zao na mabinti kutupenda
 
Tupo Inyala hapa..Tumepania kuwatumikia wananchi kwa moyo wa upendo na hata wananchi wasilslamike kuhusu wake zao na mabinti kutupenda
Kuwa serious kwa sababu tunahitaji huduma zenu. Tutakuja Inyala kupata huduma! Tusipowakuta, tutalalamika na mtajisikia mmechafuliwa jina!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…