Wakurugenzi wa Wilaya watoke maeneo husika

Kadoone

Senior Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
138
Reaction score
109
Wakuu napendekeza wakurugenzi wateuliwe kutoka kwenye maeneo husika ili kuwa na uchungu wa pesa za miradi zinazotolewa kwenye maeneo husika. Hii ya kuletewa mkurugenzi asiye mwenyeji wa eneo husika inachochea ubadhirifu wa pesa za maendeleo.
 
Mfumo upo kinafiki sana, mkurugenzi mtendaji anateuliwa na Rais na analipwa mshahara, madiwani wanaosimamia maendeleo wanachaguliwa na wananchi hawalipwi zaidi ya posho ndogo za vikao. Mkurugenzi anafahamu njaa za madiwani wake anawachora tu na madiwani wanafahamu ulaji wa mkurugenzi na idara zake kwa hiyo wote wanachorana tu!
 
Kuna maeneo yatakosa wakurugenzi kwa kukosa sifa stahiki.Umewahi kufikiria hilo?
 
Wakuu napendekeza wakurugenzi wateuliwe kutoka kwenye maeneo husika ili kuwa na uchungu wa pesa za miradi zinazotolewa kwenye maeneo husika. Hii ya kuletewa mkurugenzi asiye mwenyeji wa eneo husika inachochea ubadhirifu wa pesa za maendeleo.
Naunga mkono hoja hawa ndio watwndaji wakuu wa hlamshauri lazima waws wazawa wa eneo husika ili wapambanie kuinua halmashauri zao.
 
Wakuu napendekeza wakurugenzi wateuliwe kutoka kwenye maeneo husika ili kuwa na uchungu wa pesa za miradi zinazotolewa kwenye maeneo husika. Hii ya kuletewa mkurugenzi asiye mwenyeji wa eneo husika inachochea ubadhirifu wa pesa za maendeleo.
Ikibidi wapigiwe kura
 
Mfumo upo kinafiki sana, mkurugenzi mtendaji anateuliwa na Rais na analipwa mshahara, madiwani wanaosimamia maendeleo wanachaguliwa na wananchi hawalipwi zaidi ya posho ndogo za vikao. Mkurugenzi anafahamu njaa za madiwani wake anawachora tu na madiwani wanafahamu ulaji wa mkurugenzi na idara zake kwa hiyo wote wanachorana tu!
Madiwani wanalipwa Tena wapo mkeka wa serikali kuu(Central Gov)
 
Maeneo Husika ? Kwamba kuna wakurugenzi ambao sio watanzania ? Naona Utaifa walioanzisha Waasisi tunaanza kuuacha...;
 
Kama Mwanasiasa anaweza kuiba pesa akaenda kuwekeza nje ya Nchi, kuchagua wakurugenzi toka maeneo husika haiwezi kuwa suruhu.

Dawa ni kufumua mifumo tuliyonayo ya kimahakama, serikali na Bunge. Kupitia katiba mpya, anayetapanya mali ya umma afungwe maisha tu. Anayepokea na kutoa rushwa anyongwe.

Tuwe na sheria ngumu kama Nchi ndio tutatoboa.
 
Cheo cha DED kifutwe, hakina maana kwa wakaazi wa eneo la wilaya.

DC anatosha , tena awe anachaguliwa na wananchi na, akivurunda wananchi wawe na mamlaka ya kumuondoa kwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Majukumu kama Masuala ya ulinzi na usalama yasimamiwe na Polisi pamoja na usalama wa taifa chini ya DSO

Ili huyu mkuu wa wilaya aweze kutumie muda wake kufuatilia maendeleo, asishiriki ktk siasa, kuitwa kuitwa Dodoma na vyama vya siasa, kukimbiza mwenge wa uhuru bali atumie siku 365 za mwaka kutumikia wananchi .

Shughuli ya wilaya kuwakilishwa Bungeni na serikali kuu iwe ni kazi ya mbunge wa kuchaguliwa ndiyo awe anakimbia kimbia Dodoma kuwakilisha wilaya nzima tena, namba ya wabunge ipunguzwe iliyopo sasa iwe sawa na wilaya zilizopo kwa ujumla wabunge wote nchini Tanzania wasizidi 150.

TOKA MAKTABA :

SINGIDA: CCM YASEMA HAINA IMANI NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA SINGIDA, YATAKA AWAJIBISHWE

View: https://m.youtube.com/watch?v=LVlKRoHjMWc
 
Ilikuwa walau kwa mbaali sana rahisi wakati ule wa sera za "kishamba" na kinafiki za ujamaa , lakini kwa ubepari ni ngumu mno kumanage fedha za uma kwa ujumla wake
 
Wakuu napendekeza wakurugenzi wateuliwe kutoka kwenye maeneo husika ili kuwa na uchungu wa pesa za miradi zinazotolewa kwenye maeneo husika. Hii ya kuletewa mkurugenzi asiye mwenyeji wa eneo husika inachochea ubadhirifu wa pesa za maendeleo.
Hilo ni hitaji la Katiba mpya.
 
Wakuu napendekeza wakurugenzi wateuliwe kutoka kwenye maeneo husika ili kuwa na uchungu wa pesa za miradi zinazotolewa kwenye maeneo husika. Hii ya kuletewa mkurugenzi asiye mwenyeji wa eneo husika inachochea ubadhirifu wa pesa za maendeleo.
Kabla hujashauri hivyo,Fanya utafiti zaidi kwa kupata uzoefu wa mfumo wa counties wa Kenya.
Kule mfumo huo umeimarisha ukabila,ufisadi usiweza kuondosheka na Ajira za kikabila.
 
Back
Top Bottom