Kweli huko ukuriani ni habari nyingine.
Sasa kuna jamaa zangu huko ungonini. Niliposoma ushujaa wa wangoni au wanguni (sijui tofauti yake) nilitegemea wangoni ndio watu hapa TZ wangekuwa wakali kutetea maslahi yao hao wakurya wakasome.
Kinyume chake ni mbingu na nchi. Kuna siku nili wauliza wangoni marafiki zangu, inakuwaje mpo hivyo?
Mmoja wao alisema ni madhara ya Mjerumani kunyonga machifu hadharani huku raia wangoni wakishuhudia.
Toka siku hiyo wangoni wakachagua kuwa wapole wapole maisha yasonge mbele.
Kuna faida raia wakiwa wapole wapole, japo walichofanya wajerumani ni jambo baya sana.
Samahani wangoni marafiki zangu kama nimewakwaza.