POTOSHI Wakuu hii picha ni CHADEMA wakisomba watu kwenye mikutano huko Mbeya kama anavyosema Mohamed Kawaida?

POTOSHI Wakuu hii picha ni CHADEMA wakisomba watu kwenye mikutano huko Mbeya kama anavyosema Mohamed Kawaida?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1782451047147.png
 
Tunachokijua
Tarehe 23, 2026 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilifanya mkutano wa hadhara Mbeya mjini ambapo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii chama hicho kilieleza kuwa ni Operesheni Katiba Mpya, Free Tundu Lissu ambapo iliambatana na ofisi za chama mkoani humo.

Kadhalika Chama hicho kilichapisha picha zinazoonesha wafuasi waliohudhuria kwenye mkutano huo Rejea hapa na hapa.​

HLgeDWkW8AAzYQ_


Madai

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohammed Ali Kawaida alichapisha picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikionesha msafara wa magari huku wafuasi wa CHADEMA wakionesha bendera za cha hicho ambapo Kawaida anasema "Hivi ndivyo ndugu zetu walivyosomba Punda na Farasi kwenda kujaza kwenye mkutano wao, uliofanyika Mkoa wa Mbeya"


Je, ni kweli picha hiyo ilipigwa Mbeya?


Katika chapisho la kawaida, sehemu ya maoni mtu mmoja alijibu madai yaliyohusishwa na picha hiyo akisema "Hapo umelishwa matangopori ndugu mkiti wa UVCCM, Isakalilo ni Iringa mjini huko siyo Mbeya mjini,na walimpokea Makamu mwenyekiti wa CHADEMA taifa siku hiyo na kesho yake akampokea Msigwa , kwa hili la leo uliloandika ndugu mkiti wa UVCCM ni uongo uongo wa mchana kweupe kabisa. "

Kadhalika ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia Reverse Image Search umebaini picha hiyo ilichapishwa na kituo cha radio cha Nuru FM kutoka Iringa tarehe 12, June 2026 na kueleza kuwa ni wakati ambapo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara , John Heche alipowasili na kupokelewa na wanachama wa Chadema Jimbo la Iringa Mjini Mkoani Iringa kwa ajili ya kufanya ziara na kuhutubia wanachama na wakazi wa Iringa.

Vilevile gari ya usafiri wa umma (daladala) iliyopo katika msafara huo imeandikwa 'Isakalilo' jina ya ruti inayofanya safari zake ambapo kupitia google map inaonesha eneo hilo linapatikana mkoani Iringa.​

1782454229250-png.3616021

Hivyo JamiiCheck imejiridhisha kuwa picha hiyo imepotoshwa muktadha wake kwani haikupigwa mkoani Mbeya kama ilivyodaiwa bali kutoka mkoani Iringa wafuasi wa CHADEMA wakimpokea John Heche siku moja kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani humo.​
Mtu fulani tu mwenye kacheo mahali fulani tu ila tabia za hovyo hovyo sijui anatoa wapi
 
hao bawacha wana propaganda kitoto , huhitaji kuwa na akili kujua kuwa hawana lolote!
 
Back
Top Bottom