Wakuu hivi bei za kusuka motor zikoje

Laki tano unasuka.
Kuhusu RPM sikushauri uiongeze itakusumbua, hasa overheat and torque.

Kama mahitaji yako ni rpm 2900, tafuta mota mpya yenye uwezo huo. Kuna kiwango cha rpm kuongezeka kulingana space. Motor ya rpm 1350, unaweza upeleka bila kuzidi 1750. Changamoto huwa ni overheating.

Ushauri: Nunua mota mpya yenye rpm unayotaka, ya kusuka itakusumbua kw lengo la kuongeza rpm.
 
Aha sawa mkuu,unashauri nikisuka rpm iwe hiyo 1750 au
 
Huku kwetu waya copper mita elfu 43 kwenye mota ya 15hp nadhani zinaingia kilo 7 hivi, ufundi laki 1 so andaa laki 5 unasuka hiyo mota. Kikubwa usiongeze wala kupunguza chochote isukwe irudi kama awali
 
Ni mashine ya kubaraza, acha speed ya motor,yenyewe ina speed ya 3500 rpm

Kama ni mashine ya kubaraza, rpm 1750 inaweza zungusha 3500 rpm ya kinu bila shida kabisa. Cheza na puli na mikanda.
Tumia pulley ya nchi nne kwenye mota, tumia mkanda mrefu V-Belt 120.
Pulley ya mashine ya kubaraza kama ni nchi 10, ipunguze tumia nchi tano.
 
Hamna mkuu pulley ya mashine ya kubaraza ni inch 4 kukaribia tano,na ya motor inayosumbua ni 7 inch
 
Kwa mota used aina yoyote 0768010493 pia rewinding services zinapatikana mfano
 

Attachments

  • IMG_20261014_174211_239.jpg
    811.3 KB · Views: 4
  • IMG_20260929_101346_781.jpg
    643.4 KB · Views: 5
  • IMG_20260925_133015_453.jpg
    962 KB · Views: 6
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…