WB na IMF ni vyombo pekee katika Uchumi wa dunia. Hauwezi ukatunga tuu chombo kingine kufanya kazi hizo. Zina kazi mbili;
1. IMF
Mataifa yanapofanya biasahara kuna kitu kinaitwa Mizania ya Biashara (balance of trade). Nchi moja inaponunua vitu vingi kuliko inavyouza nje, inleta hali ya hii nchi kubidi kukopa kulipia hii ziada. Kimsingi hii siyo mbaya - mpaka pale madeni yanapokuwa makubwa mno. Ikitokea hii, hiyo nchi hupoteza uwezo wake wa kukopa na kwa hiyo wadeni wake nao wanaumia. Uchumi wa dunia unakuwa hatarini.
Kazi ya IMF ni kukopesha kwa mataifa yaliyofikia hatua hii ya kutokopeka. IMF inapokukopa hela, itakuambia ubadilishe namna unavyoishi, ili uweze kurejesha uchumi wako katika hali nzuri. Watakuambia uache kununua vitu nje, uongeze uzalishaji, upunguze matumizi yasiyo na msingi. Masharti haya ndiyo yanafanya watu wasizimie sana IMF - lakini wanapaswa kukumbuka kuwa wamejiweka katika halii hii wenyewe kwa kuendekeza anasa.
2. World Bank
World Bank ipo kwa ajili ya kutoa misaada kwa mataifa ambayo ni mazembe tu. Mataifa ambayo yameshindwa kutoa huduma kwa wananchi wake, k.m elimu, afya, miundombinu. Missada hii hulenga zaidi kuleta ahueni kwa wananchi - na ndiyo maana watu wanaipenda-penda WB.
WB na IMF zipo kikazi zaidi. Hazipo kwa ajili ya kugawana vyeo. Vyeo ni lazima vijazwe, lakini utaonekana ni mtu wa ajabu sana ukitoka kwenye nchi iliyoshindwa kujiendesha na kuanza kudai eti unataka MD awe anatoka kwenye nchi zembe.