Wakuu hivi watengeza ugoro huwa wanachanganya nini mpaka unakuwa mkali sana?

Mkuu,

Unataka ugoro upi uwe mkali? Maana kuna aina mbili au tatu za ugoro.
1. Ugoro wa kuvuta puani 2. Ugoro wa mdomoni 3. Ugoro wa kunako kwa wanawake.

Jinsi ya kutengeneza ugoro mkali.
1. Chukua tumbako kavu, weka jikoni upashe upate joto. Tunafanya hivi kwa sababu tumbaku huwa unalegea kiaina. Ukipasha unakuwa rahisi kuutwanga.

2. Ukishapata joto, chukua weka kwenye kinu. Anza kuutwanga. Ukilainika mimina kwenye nguo nyepesi, anza kuchuja. Hii itakusaidia vumbi lake tu kupatikana. Ile baki rudisha kwenye kinu na anza kutwanga tena. Na urudie zoezi mpaka umalize.

3. Chukua magadi yako kiasi. Kulingana na ukubwa wa tumbaku yako uliyosaga. Magadi ndiyo huamua haswa ukali wa ugoro. Weka jikoni upashe joto kidogo. Kisha nao utwange ili ibaki vumbi kama ulivyofanya awali kwenye tumbaku. Kisha uchuje kwa kitambaa kisafi.

4. Chukua tumbaku uliyosaga na magadi. Changanya kwa pamoja kwa mikono yako mpaka uhakikishe umechanganyika vema.

5. Chukua mafuta ya kula. Hakikisa haina mabonge. Kama yapo basi tia jikoni upashe. Kisha mwaga kwenye ule mchanganyo wako. Changanya vizuri.

Kuwa makini sana kwenye uwekaji wa mafuta. Ukiweka mengi yanakamatana sana. Hivyo weka kidogo alafu unasikilizia ukishachanganya.

6. Hapo kwenye mafuta, wengine huamua kuweka vingine. Badala yake, huamua kuweka mkojo wa binadamu asiyekunywa maji. Anaenda anamkingia kisha anamletea.

Ule mkojo wa njano, unakuwa na chumvi kali sana. Akiuchanganya unakuwa mkali mno.

Lakini si vizuri, kitu ambacho mwenzako anauweka mdomoni uweke mkojo wa mtu mwingine.

Kuna majani mengine yapo huko umasaini. Sijayaona kwingine. Ila ugoro ukiwekwa unakuwa unawasha mdomoni kama mint.

Kumbuka, ugoro ni HATARI kwa afya yako. Una addiction kali zaidi ya sigara. Jihadhari usiutumie.

Kila la kheri.
 
Ugoro ninavyojua ni yale majani ya tumbaku ndo hayo yanasindikwa.

La kujua tu ni kuwa ukali wa ugoro unategemea eneo, udongo mwingine unazaa tumbaku kali udongo mwingine laini.

Unless otherwise anaongeza bange.

Don't use, ni hatari kwa afya yako
 
Unaongeza km unavyoongeza chumvi kwenye mboga na ni lazima uonje sio unawekaweka tu utawipikia wenzio Sumu uwaue, km kitu huwezi tafuta wanaojua wanaopika ugoro hua wanaonja radha je umekolea au waongeze viambata ni km mapishi, sio wewe hutumii ugoro unataka kuwapikia wenzio madalanzi utaua watu shauriyako utawatengenezea Sumu uwaue kwa tamaa zako za kijinga
[emoji16][emoji16]
 
Ndio sio bia tu hata kwenye juice au soda ukichanganyiwa subiria maelezo Ila upate ugoro mkali Grade A fukuto ule ambao hata ukisikia harufu yake tu unajisikia kunyakunya hapo haujautia mdomoni au puani
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kilimo Cha tumbaku Tabora sikonge, kule wanauza ugolo Sana masokoni Mi naona ugolo ni mzuri kwa matumizi kuliko mibangi au milungu,
Acha kufananisha milungi na uchafu
 
Mkuu,

Unataka ugoro upi uwe mkali? Maana kuna aina mbili au tatu za ugoro.
1. Ugoro wa kuvuta puani 2. Ugoro wa mdomoni 3. Ugoro wa kunako kwa wanawake.

Jinsi ya kutengeneza ugoro mkali.
1. Chukua tumbako kavu, weka jikoni upashe upate joto. Tunafanya hivi kwa sababu tumbaku huwa unalegea kiaina. Ukipasha unakuwa rahisi kuutwanga.

2. Ukishapata joto, chukua weka kwenye kinu. Anza kuutwanga. Ukilainika mimina kwenye nguo nyepesi, anza kuchuja. Hii itakusaidia vumbi lake tu kupatikana. Ile baki rudisha kwenye kinu na anza kutwanga tena. Na urudie zoezi mpaka umalize.

3. Chukua magadi yako kiasi. Kulingana na ukubwa wa tumbaku yako uliyosaga. Magadi ndiyo huamua haswa ukali wa ugoro. Weka jikoni upashe joto kidogo. Kisha nao utwange ili ibaki vumbi kama ulivyofanya awali kwenye tumbaku. Kisha uchuje kwa kitambaa kisafi.

4. Chukua tumbaku uliyosaga na magadi. Changanya kwa pamoja kwa mikono yako mpaka uhakikishe umechanganyika vema.

5. Chukua mafuta ya kula. Hakikisa haina mabonge. Kama yapo basi tia jikoni upashe. Kisha mwaga kwenye ule mchanganyo wako. Changanya vizuri.

Kuwa makini sana kwenye uwekaji wa mafuta. Ukiweka mengi yanakamatana sana. Hivyo weka kidogo alafu unasikilizia ukishachanganya.

6. Hapo kwenye mafuta, wengine huamua kuweka vingine. Badala yake, huamua kuweka mkojo wa binadamu asiyekunywa maji. Anaenda anamkingia kisha anamletea.

Ule mkojo wa njano, unakuwa na chumvi kali sana. Akiuchanganya unakuwa mkali mno.

Lakini si vizuri, kitu ambacho mwenzako anauweka mdomoni uweke mkojo wa mtu mwingine.

Kuna majani mengine yapo huko umasaini. Sijayaona kwingine. Ila ugoro ukiwekwa unakuwa unawasha mdomoni kama mint.

Kumbuka, ugoro ni HATARI kwa afya yako. Una addiction kali zaidi ya sigara. Jihadhari usiutumie.

Kila la kheri.
Mkuu shukrani sana hapa umenipa mwanga nitengeneze mwenyewe
 
Hapa naiona fursa . Nawaza kuutengeneza kisasa kidogo zitoke kama pipi flani hivi isiwe kwenye form ya unga
 
Mwanangu ugoro unafaida Mimi naagiza wa 25elfu na nikiufunga unatoa pic 60+ na Kila pic ni elfu 1 na Kwa wiki naweza agiza zaidi ya mara mbili kwahiyo uhakika wa 50elfu per week unakuwepo... Pesa ya Kodi ya meza na matumizi madogo ya familia tayari
 
Hapa naiona fursa . Nawaza kuutengeneza kisasa kidogo zitoke kama pipi flani hivi isiwe kwenye form ya unga
Kikubwa tu uwe na jina eneo husikia...na jina unalitengeneza Kwa kuwa na mzigo mzuri mkaliii kuwazidi washindani wako na hiyo itakufanya mzigo ukiufunga unauuza Kwa uharaka unawahi kuisha unaagiza mpya mwingine maana ugoro hautakiwa ukae muda sana unapoteza ubora. Na ukipoteza ubora unapoteza wateja pia
 
Kwa huku wanaita" dawa" hivi kwanini waga wanatema mate wakati wamemeza kwa hiariii🤔🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom