Ni kweli, wakuu akenajo & mtu kitu, mmetoa jibu sahihi: Hata hivyo acha niongeze jamb moja tu!
Mboga[SUP]1[/SUP] = mmea unaotambaa wenye majani mapana ambao huzaa maboga na majani yake huliwa kama mboga.
Mboga[SUP]2[/SUP] =kitu cha kutowelea chakula kama vile nyama, maharage au samaki.
Kulingana na kamusi ya Kiswahili Sanifu, 2009.
*Jambo la kukumbuka ni kwamba matumizi ya maneno katika lugha yoyote hubadilika baada ya wakati fulani kupita.
Mfano:
Katika Kiswahili[Kulingana na ufafanuzi wa BAKITA],
Kiate = mtoto ambaye amefiwa na wazazi wake wawili.
Mwana mkiwa = mtoto ambaye amefiwa na mama.
Yatima= mtoto ambaye amefiwa na baba.
Lakini kwa matumizi ya sasa ya Kiswahili, utaona watu wengi hutumia neno "yatima" zaidi kuliko hayo mengine.
Ukirudi kwenye tofauti ya mboga na kitoweo, jibu liko wazi:
mboga = za majani[vegetables kwa Kiingereza] + maharage + jamii ya kunde.
kitoweo = kuku, ng'ombe, mbuzi, samaki n.k.
Lakini si ajabu kuona watu wakitumia neno "mboga" katika hali zote!:smiling:
"Take the attitude of a student, never be too big toask questions, never know too much to learn something new"