Wakuu ipi sahii?

Wakuu ipi sahii?

skendo

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
212
Reaction score
102
Heshima kwenu wakuu.tumekua na mabishano na wenzangu hapa kazini kwa mda mrefu sasa kwani kila mtu amekua akitoa tafsiri yake katika hili.
Issue ni hii.
Neno mboga tafsiri yake ni ipi?maana wengine wanasema mboga ni zile za majani tu mfn.mchicha,chaina nk. ila huwezi kuita nyama,samaki ama uyoga mboga.ila samaki,nyama ni vitoweo haziwezi kuwa mboga isipokua tunaita mboga kimakosa
jamani hoja hii ni kweli?kwa wale wenye ujuzi wa kiswahili msaada tafadhali
 
MBOGA : zina asili ya majani / miti

KITOWEO : nyama na samaki
 
Mboga ni zile zinazotoka shambani ,sio mifugo au baharini
 
Ni kweli, wakuu akenajo & mtu kitu, mmetoa jibu sahihi: Hata hivyo acha niongeze jamb moja tu!

Mboga[SUP]1[/SUP] = mmea unaotambaa wenye majani mapana ambao huzaa maboga na majani yake huliwa kama mboga.
Mboga[SUP]2[/SUP] =kitu cha kutowelea chakula kama vile nyama, maharage au samaki.

Kulingana na kamusi ya Kiswahili Sanifu, 2009.
*Jambo la kukumbuka ni kwamba matumizi ya maneno katika lugha yoyote hubadilika baada ya wakati fulani kupita.
Mfano:
Katika Kiswahili[Kulingana na ufafanuzi wa BAKITA],

Kiate = mtoto ambaye amefiwa na wazazi wake wawili.
Mwana mkiwa = mtoto ambaye amefiwa na mama.
Yatima= mtoto ambaye amefiwa na baba.
Lakini kwa matumizi ya sasa ya Kiswahili, utaona watu wengi hutumia neno "yatima" zaidi kuliko hayo mengine.

Ukirudi kwenye tofauti ya mboga na kitoweo, jibu liko wazi:
mboga = za majani[vegetables kwa Kiingereza] + maharage + jamii ya kunde.
kitoweo = kuku, ng'ombe, mbuzi, samaki n.k.

Lakini si ajabu kuona watu wakitumia neno "mboga" katika hali zote!:smiling:

"Take the attitude of a student, never be too big toask questions, never know too much to learn something new"
 
Nadhani kama alivyosema aliyetangulia hapo juu kwamba matumizi ya maneno hubadilika kulingana na wakati.Na kwa jinsi nijuavyo mimi neno mboga ukilitumia kwa wakaazi wa Dar, moja kwa moja watalielewa katika maana zote mbili (KITOWEO,- MBOGA)na watalielewa kirahisi bila tabu yoyote kulingana na mfumo wa maongezi utavyokuwa.Kiufupi mboga siyo tu ya majani na wala siyo tu kitoweo. Linategemea vipi na wapi limetumika
 
Back
Top Bottom