Wakuu Kifo Sasa nje nje chukua tahadhari

Wakuu Kifo Sasa nje nje chukua tahadhari

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Wakuu toka mwezi huu uanze nimesikia vifo vya watu ninaowajua Zaid ya 10.hali inatisha Sana naona watu wengi Sana wana danja.israeli hajatumwa kumaliza Tena watu kwa gharika au Moto Sasa hivi anakuja kukuchukua jumla jumla yaani hata nafasi ya kuumwa na kulazwa ndani ya week hutapata anakuja kukuchukua mzima mzima.unaweza ukaumwa TU kichwa ukafa.vifo vya ghafla ukiumwa Sana Ni siku mbili tu.kwa hiyo nawapa tahadhari muwe makini sana dunia imekuwa na watu wengi Sasa inaamua kupunguza kadhaa.siwatishi lakini nawasihi TU muwe makini hakikisha muda wote unakuwepo sehemu salama na unakuwepo muda sahihi.mwezi wa pili wa tatu na wa nne na wa tano jitahidi Sana urudi kwenye ibada.watu wanaondoka mpaka sio poa.na hasa vijana kwa sababu hatusikii
 
Kwa hiyo ibada ni kwa woga wa kufa au ni njia ya maisha?Ishini kadiri impendezavyo Mungu na jirani.Kuishi na kufa ni kanuni ya kimaumbile "chochote kiishicho kitakufa kama ambavyo kilicho kufa kitaishi.Ukamilifu wa uhai upo katika kifo kama ambavyo kifo kinakamilishwa na uhai.Hivi ni vitu visivyo tengana kamwe vi pamoja daima tunatambua uhai kwakuona mtu/mmea,myama hai lakini tumbue kifo pia ki sehemu ya uhai huo.Hivyo usiogope kufa ni hakika na hakiondolewi kwa watu kuogopa.Jitahidi kuishi vizuri na wenzio ili ukifa uendelee kuishi mioyoni mwao.Usisali sababu utakufa bali sali kwa sababu ndio njia muafaka ya kutuliza hofu zetu juu ya kifo,lakini pia njia muafaka ya kujulisha nia yetu njema ya kushirikiana na kusaidiana na wenzetu(mpendane kama nilivyo wapenda).Usijae hofu,pambana ushinde hofu ya kifo na woga wa mauti ili uishi hata baada ya kifo chako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni njia mojawapo ya Mungu kutuonesha kuwa duniani si makao yetu ya kudumu.

Wanadamu tuna mioyo magumu sana, maana tungekuwa tunajifunza kupitia kifo/vifo vya ndugu, jamaa na rafiki zetu ;basi ibada zetu na unyenyekevu kwa Mungu ingekuwa sehemu ya maisha yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Wakristo KUFA NI FAIDA...na tunafaa kukitamani kifo ili tukaishi na Kristo...Mtume Paulo anapiga mfano kwa andiko lake hili, Soma:

Wafilipi 1:21-25 Neno: Biblia Takatifu
21 Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida. 22 Kama nitaendelea kuishi katika mwili, hii itaniwezesha kufanya kazi yenye matunda. Lakini sijui nichague lipi! 23 Yote mawili yananivutia: natamani niyaache maisha haya ili nikakae pamoja na Kristo, jambo ambalo naona ni bora zaidi. 24 Lakini kwa sababu yenu naona kuwa ni muhimu zaidi nikiendelea kuishi. 25 Nina hakika kwamba, kwa sababu hii nitabaki na kuendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili mpate kukua na kuwa na furaha katika imani.
 
Back
Top Bottom