PSG wanatumia gharama kubwa za usajili ili walau waweze kutwaa taji la Mabingwa Ulaya (UEFA).
Pamoja na kuwa wamekuwa wakishinda taji la Ligue 1, lakini kiu kubwa ya Mashabiki ni UEFA. Bahati mbaya sana, wamekuwa wakiangukia pua kila leo.
Katika matamanio yao hayo na kufeki kwa timu, wanàmini kuna wachezaji ambao hawajitoi kuipambania timu na hawaoni thamani ya jezi za Club yao. Wanaamini Neymar ana uwezo mkubwa, lakini haonyeshi spirit ya kuipambania timu. Ni mchezaji wa tatu kwa Mshahara Mkubwa baada ya Mbappe na King Leo.
Wanaona kuwa analipwa fedha nyingi bila matokeo. Aondoke tu. Messi pia, ila kwa heshima tu ya Leo wanashindwa kumzomea. Hana muda mrefu pia klabuni kama Neymar.