Wakuu, mnifundishe kubet!

Wakuu, mnifundishe kubet!

Wakuu,

Leo nimeamka sina hata mia, ila kuna rafiki yangu hapa kanitumia mwekundu ili niweze kusogeza siku. Sasa baada ya kufikiria jinsi ya kuweza kuishi hasa katika kipindi hiki kigumu cha Magufuli, nimeonelea nianze kufanya biashara ya kubet.

Mimi sio mpenzi wa mpira na hata tangu nizaliwe (I mean since 1997) sijawahi kaa kuangalia mechi moja ya mpira ikaisha. Sasa naombeni mnipe ABC za kubet mengine nitajiongeza.Nataka niunenepeshe huu ugali ili maisha yasonge.
Acha kabisa hiyo kitu, pesa yako itapotea bure.
 
Najuta kujua kubet .siwezi kuacha kabisa hii mambo..sikushauri uingie huku hakufai kabisa.
 
Naogopa kukugundisha maana utaliwa mpaka unye
 
Bwa mdogo usipapie vitu eti kwa kuwa wengine wanafanya. betting ni kamari, na kamari haifai ingawa ipo kisheria. tofauti ya mcheza kamari na mvuta unga ni ndogo sana. katafute kazi ufanye. Ikibidi tafuta shamba ukalime kuliko kufikiria biashara ya kamari
 
Back
Top Bottom