wakuu msaada wenu muhimu hapa

wakuu msaada wenu muhimu hapa

babukijana

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2009
Posts
14,478
Reaction score
18,341
kipindi cha nyuma niliwahi kuwa na mahusiano na binti mmoja wa kimarangu hapo mujini bongo,kweli tulipendana sana na baada ya kujitambulisha kwao tu akapata mimba,baada ya hapo ikawa haina jinsi tuangalie mimba kwanza mpaka mtoto akizaliwa ndio tuendelee na mipango mingine ya ndoa,haya kilichotokea toka kipindi ana mimba binti akaanzisha visa vya ajabu ajabu nyumbani mpaka alifikia kunipeleka polisi usiku akasingizia nilimtishia kumuua,haya hayo yakaisha mimi nikaendelea tu kumvumilia nikijua labda ni mimba inamsumbua,baada ya kujifungua tu mama akaanza vituko tena si vya kawaida,ukirudi nyumbani usiku kutoka mihangaikoni unamkuta hayupo,mtoto mdogo kabisa kaachiwa housegirl,ukienda mango garden mida hiyo unamkuta na marafiki zake mda mwingine na mijamaa lakini mi nilikua na chill tu,akiniona anakuja anajidai kanifumania kesho yake yeye wa kwanza kupiga simu moshi kuwaeleza kanishindwa mara kanifumania kumbe mimi ndio nimemfuma usiku nje,haya tuachane na hayo,baadaye nikaja sikia kapata kibwana mdogo kimoja hapo kino kilikua kinauzauza unga basi ndo kinampagawisha,mi nilipoona anazidi kuniumiza kichwa nikaamua kutafuta kazi ya mbali kabisa nayeye,nikichukulia at least akinikosa kwa muda atanikumbuka,atatulia,wacha bwana,nikapata mkataba na jamaa fulani walikua wanafanya reseach ya wanyama na kupiga picha mbuga zote za kusini mwa afrika,nikapata mkataba mzuri miezi 8,baada ya kuondoka na hao jamaa huku nyuma mama ulingo ukawa wake,mtoto kambwaga moshi,ikawa ni yeye na club,club nayeye mimi ananidanganya mtoto yuko nae dar natuma pesa matumizi kilakitu,huku na kule kazini nikapata kawiki ka kupumzika namimi nikarudi dar ghafla,nikampigia simu tayari nishafika nyumbani nakuta nyumba kafunga hayupo nikiuliza majirani wakasema kwanza sikuhizi hapo akija ni kubadili nguo na kuanza,nikampigia simu hakuamini kama nipo dar,haya akarudi homu,kapiga kimini cha kufa mtu,halafu hizo dharau alizonionyesha aliporudi dooh,haya hayo yakapita siku hiyo nililazwa polisi tena baada yakubishana nae kidogo tu,nilipotoka kesho yake nikarudi homu tena yeye sasa akawa ndio mtawala nikisema jambo tu anakimbilia kunipeleka polisi,baada ya kunilaza polisi tena mara ingine nikaona sasa basi,nikaamua kuondoka kabisaaa nikaendelee na maisha kivyangu,alipoona nimeondoka huku nyuma nilikua nimeacha kila kitu nyumbani basi akasaka certificate zangu original akazichana zote,nia yake ili nilost huko nilikoenda,haya mi nikatymia uzoefu tu wa mujini nikapata kazi tena na baadae kidogo alhamdulilah nikampata binti mwingine safii ambaye sio siri alinisaidia sana kipindi hicho kimawazo na kiuwezo kwani yeye alikua anajiweza tu.huyu mama watoto nilipoachana nae akaanza kuishi na huyo jamaa yake kabisa,haya mimi niliendelea na maisha yangu sikuwajali sana licha ya yeye kuendelea kunisumbua kuja kufanya mafujo kwangu,kuniletea mapolisi nyumbani kuvunja vioo vya gari,kupasua simu zangu au kukimbia nazo,kumtukana mama yangu mzazi,na mtoto akanza kumjaza ujinga kama yule jamaa anayeishi naye ndio baba yake!,haya turudi kwenye pointi,mimi nilipoona anazidi kusumbua nikaamua kuondoka kabisa hapo tz,nikaenda ughaibuni,kufika huku kama mnavyojua nimehangaika na box na nikapata mke nimeoa,sasa bahati nzuri huyu mke wangu anapenda sana watoto na akampenda sana mtoto wangu alipoomuona tu kwenye picha,anataka tufanye jitihada za haraka mtoto aje huku asome pamoja na kukaa na sisi hapa,na anataka tukija tu huko likizo hii turudi naye,tatizo nimeongea na mamayake naona tayari kashaanza kuweka migogoro kama kawaida yake,anaanza kuongelea maswala ya pesa bila kuangalia future ya mtoto,ukizingatia mtoto hata yeye mwenyewe hakai naye kwani baada ya mimi kuondoka nayeye huwa mara nyingi yuko china kwa madai anafanya biashara,mtoto yuko kwa mdogo wake,sasa sijui nifanyeje hapo wakuu maana nimeshaona haki ya mtoto sasa inataka kunipotea hivihivi nikiwa kama baba.nishaurini
 
Pole shem lakini pia hongera ulitupa utumbo ukaachana na nzi

mtoto wenu ana umri gani?
 
Pole shem lakini pia hongera ulitupa utumbo ukaachana na nzi

mtoto wenu ana umri gani?

wakwetu una speed ya kusoma...mimi nimechemsha nimeishia njiani
 
Kwani wewe umemuwekea condition zipi kuhusu mtoto wake ,,
Nadhani hata ningekuwa mimi sijui kama ningekupa mtoto wangu --oops ma baby mmh inabidi mkae chini muongee vizuri kuhusu swala hilo
 
Kwa maelezo yako nina wasiwasi kama kweli huyu mtoto ni wako.Nahisi ulipakaziwa.
Lakini akizidi kukusumbua nenda mahakamani ukatafute haki ya kulea mtoto kwa vile ushahidi unao kuwa mama yake hamjali na unawasiwasi na future ya mtoto.bht anajua haya mambo ya sheria akufafanulie zaidi.
 
wakwetu una speed ya kusoma...mimi nimechemsha nimeishia njiani

mmh wa kunyumba afu shem hajaweka hata aya sasa....
nimejitahidi sana leo mpaka mwisho......
 
Kwa maelezo yako nina wasiwasi kama kweli huyu mtoto ni wako.Nahisi ulipakaziwa.
Lakini akizidi kukusumbua nenda mahakamani ukatafute haki ya kulea mtoto kwa vile ushahidi unao kuwa mama yake hamjali na unawasiwasi na future ya mtoto.bht anajua haya mambo ya sheria akufafanulie zaidi.

hahaaaa mi ni TAWLA na WILAC sio
Charity usisahau na wewe ni mweka hazina kule
nimeanza kumuuliza shemeji umri wa mttoto lakini pia angalizo ulotoa ni la muhimu kuhusu ukweli kuwa je mtoto ni wake?? it can be proved though....
 
Kwahiyo mkeo ndo analazimisha mtoto muende nae ughaibuni, wewe hutaki!

Kumbuka huyu mkeo hakuwepo wakati unakutana na kasheshe ya huyu mama!
All in all, mtoto hatopotea, however!
 
Kwahiyo mkeo ndo analazimisha mtoto muende nae ughaibuni, wewe hutaki!

Kumbuka huyu mkeo hakuwepo wakati unakutana na kasheshe ya huyu mama!
All in all, mtoto hatopotea, however!
Tatizo hapa mama yake mzazi wa mtoto ni kirukaruka.na huyo mtoto anahitaji kujengewa future nzuri mapema.mie naona ni bora afanye la kufanya amchukue mtoto amtunze.
 
Babu kijana edit kidogo hii thread iwe user friendly!!
 
hahaaaa mi ni TAWLA na WILAC sio
Charity usisahau na wewe ni mweka hazina kule
nimeanza kumuuliza shemeji umri wa mttoto lakini pia angalizo ulotoa ni la muhimu kuhusu ukweli kuwa je mtoto ni wake?? it can be proved though....
Tutashirikiana tu kuhakikisha haki inatendeka.lakini wewe si ndio stering,mie natoa tu mafungu ya safari.
Na huyu mtoto DNA ni ya muhimu ingawa wanasema kitanda hakizai haramu.........
 
Kwa maelezo yako nina wasiwasi kama kweli huyu mtoto ni wako.Nahisi ulipakaziwa.
Lakini akizidi kukusumbua nenda mahakamani ukatafute haki ya kulea mtoto kwa vile ushahidi unao kuwa mama yake hamjali na unawasiwasi na future ya mtoto.bht anajua haya mambo ya sheria akufafanulie zaidi.
kuhusu mtoto sina wasiwasi nae kabisa kwamba sio wangu mama wengine huwa hatupakaziwi.
 
Kwanza kacheki DNA kwanza.. kama inawezekana ili ujue mtoto ni wako kweli.. Then hangaikia kuondoka nae.
 
Kwahiyo mkeo ndo analazimisha mtoto muende nae ughaibuni, wewe hutaki!

Kumbuka huyu mkeo hakuwepo wakati unakutana na kasheshe ya huyu mama!
All in all, mtoto hatopotea, however!
hapana mkuu nilikua nataka sana lakini si unajua hawa wenzetu huwezi kuwatangulizia hilo ila yeye mimi nilipomwambia nina mtoto bongo ndio alikua wa kwanza kusema tufanye mpango aje,tena alienda mpaka huko moshi kumuona na kumsalimia mama yake akakataa kumpeleka hotelini.
 
Kwanza kacheki DNA kwanza.. kama inawezekana ili ujue mtoto ni wako kweli.. Then hangaikia kuondoka nae.
kaka,mama, mtoto shaka ondoa ni wangu kabisaaa,hilo sio swala la kuuliza tuendelee na mjadala.
 
Kwanza kacheki DNA kwanza.. kama inawezekana ili ujue mtoto ni wako kweli.. Then hangaikia kuondoka nae.
Ivi siku izi kucheck DNA hakuna mlolongo? maana nasikia sijui mpaka upate kibali polisi au mahakamani? with concrete reason?
 
umri una ruhusu mtoto kuishi na baba
hehehhee.Nakuaminia cheapesoni wangu...........
Sasa tuendelee na mchakato wa kumpeleka mtoto kubeba boksi....
Na BK kadhibitisha huyu mtoto ni damu yetu.
 
Back
Top Bottom