Wakuu, mwenye uzoefu kuhusu ujenzi wa nyumba

Wakuu, mwenye uzoefu kuhusu ujenzi wa nyumba

Varbo, wewe ukisikia nyumba ina room 4, unafikiri vyote vina ukubwa sawa?
 
Last edited by a moderator:
Haikutajwa Vinne tu imeorodheshwa na unapoambiwa makadilio sio idadi kamili!! Nadhani wewe Ndio hujaelewa
 
Kwahiyo nyumba itakua
1.tofali 3000@tsh 700/=
2.mchanga roli 3@tsh 250,000/=
3.kokoto roli 2@tsh 250,000/=
4.cement mifuko 200@tsh 15,000/=
5.bati 80@tsh 16,000/=
6.mbao,misumari,gypsumboard,tiles,rangi,vioo,jumla tsh 11milions
7.ufundi tsh 6milions
8.finish materials tsh 7milions.


Huu ni ushauri wa kukatisha tamaa mtu asijenge. Labour charge 6mill?.
 
Cha muhimu sana hapo pesa ya kuanzia.TZS Mil40 lazima uwe nayo mkononi,gharama nyingine zinakuja taratibu as you go
 
Cha muhimu sana hapo pesa ya kuanzia.TZS Mil40 lazima uwe nayo mkononi,gharama nyingine zinakuja taratibu as you go

kwa kiasi hicho sidhani kama watu tungejenga....
 
Huu ni ushauri wa kukatisha tamaa mtu asijenge. Labour charge 6mill?.

Kwanza hiyo aliyosema ni ndogo! Kama anaanzia chini kabisa yaani msingi hadi jengo kwisha na finishing yake, gharama za kuwalipa mafundi wa fani mbalimbali, asipokuwa makini hadi jengo linaisha hawezi kubakiwa hata na senti ya yeye aliyechukua kazi, hela zote watachukua mafundi! Million6 wala hajakupiga! Labour charge ni 10-15% ya gharama za ujenzi. Wakati mwingine kutegemeana na mazingira, ugumu na vikwazo mbalimbali, hufika hadi 20%
 
Cha muhimu sana hapo pesa ya kuanzia.TZS Mil40 lazima uwe nayo mkononi,gharama nyingine zinakuja taratibu as you go

Akipigiwa sana haya mahesabu ya gharama za ujenzi, mwisho itamletea uoga na akashindwa kujenga. WaTZ huwa tunaanza kibongobongo, ikifika kwenye lentel unapumzika unaendelea kujikusanya (hata ukiwa sehemu unapata moja bariiiiiidi unajiona uko safi kabisa). Nguvu ikija unaendelea taratibu utajikuta umepiga bati, hapo furaha inazidi kuongezeka. Baada ya kama miaka mitatu au minne hivi (kutegemeana na income ya mtu) unaingia lakini bado kuna mambo madogomadogo utaendelea kupambana nayo humohumo. Hii ya mara QS, sijui Archtect, Structural Engineer, Building Economist nk waje wakupe pressure bure hadi ujikute unalazimisha kutengeneza ka-EPA hata nyumba haijaisha uko Segerea (Labda kama mleta maada siyo wakusubiri tarehe 30, ingawa wale wasiosubiri tarehe 30 huwa hawajiulizi waanzeje kujenga).
 
wewe kama una hata mil 2 tafuta ramani.. anza kuchimba msingi...haya magarama yasikutishe...
mjini mipango....
 
Mavuno Nyamanoro. ukowapi uje utoe msaada na ushauri. kunajamaa yuko humu anaitwa (Mavuno Nyamanoro) kasaidia wengi sana. Imail yake ni anapatikana kwa 0756 156 828( kombaemmanuel42@gmail.com ) ukimupata ujue umejenga.
 
Nahitaji kujenga nyumba kwa sasa,idadi ya vyumba ni vinne, jiko, store, public toilet,vyote ndani kwa ndani" msaada unahitajika hapa

1:kwa makadirio ya jumla niandae tsh. ngapi mpaka nyumba kukamilika.

2:kwa wale wataalam wa kupaua(kupiga bati) ni kiasi gani cha bati kitahitajika hapo, just by makadirio tu.bila kusahau idadi ya mbao.

Ni hayo tu wakuu eneo la ujenzi lipo Tanga mjini.

Mkuu Unayo Ramani?Kama hauna ramani, Mamlaka ya Jiji si wasumbufu kwa Ramani Itakayochorwa nje ya Tng?Jibu hayo nikusaidie makadirio hadi Ramani mkuu takutumia hata kwa Raha Leo Au Simba
 
Huu ni ushauri wa kukatisha tamaa mtu asijenge. Labour charge 6mill?.

Hajamkatisha tamaa amempa makadirio tena hiyo yaweza kupungua au kuongezeka kulingana na ubora na mbwembwe zitakazowekwa humo ndani
 
weka ramani ya nyumba unayotaka ndio tuweze kufanya makadirio ya vifaaa na gharama
 
iko sababu ya kumueshimu mume kama yeye ndo kakuingiza mjengoni
 
Huu ni ushauri wa kukatisha tamaa mtu asijenge. Labour charge 6mill?.


Hiyo kweli mkuu tena hapo naona kama ndogo, ila uzuri wake sio kwamba unalipa at par, ni unalipa kidogo kidogo hata kuanzia 200,000/= au 100,000/= kwa siku ambazo mafundi wanajenga. Cha muhimu ni kuhakikisha kuwa sio unampa hela yote fundi. na hata kama una hela unaongea na fundi kwamba utampa siku fulani hivi kama wewe ni wa tarehe 30. Vilevile unaweza hata kuongea na wenye vifaa vya ujenzi ukakopa kidogo kidogo na kuja kulipa baadaye. Kwingine tu msingi na kupandisha mpaka lenta na kozi mbili za juu si chini ya milioni nne na nusu. Bado hujaongezea gharama za kupaua na zile finishings zingine zingine.

Balaaaa
 
Back
Top Bottom