Wakuu naomba kuelimishwa kuhusu imani/dini ya Rastafarians

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Habari wakuu,

Ningependa kuelimishwa haya machache kuhusiana na hii imani/dini ya Rastafarian (nikipata kujuzwa na ya ziada ntashukuru sana).

1. Naskia rastafarian hawanywi pombe hivi Ni kweli? Kama ni kweli je, ni kwanini?

2. Nasikia hawali kitimoto je, kweli? Kwanini?

3. Nasikia ni marufuku kuhudhuria au kulia msibani je, ni kweli? Kama ni kweli kwanini? Wao rastafarian wakifariki nini kinafanyika? Hawazikwi au inakuaje?

4. Naskia kuvuta bangi kwao ni sehemu ya ibada je ni kweli? Kama ni kweli kwanini? Hivi ni lazima ukiwa rastafarian uvute bangi?

5. Hawa rastafarian mtume wao ni nani Kama ilivo kwa Islamic (Mohammad) Chirstian (Yesu).

6. Hawa rastafarian wanacho kitabu kitakatifu Kama ilivo kwa christians (Biblia) na Islamic (Quran)

7. Nasikia kwa rastafarian ni marufuku kula nyama nyekundu wala mayai ni kweli? Kama ni kweli kwanini?

8. Hawa rastafarian wanazungumziaje habar za kufa, kifo na habari kufuliwa upya uko mbinguni?

9. Hawa rastafarian wanazungumziaje kuhusu wale wanaotenda yale mema & mabaya hapa Duniani, malipo yao itakuaje uko mbinguni. Yaani kwao imani yao mema ni yapi na mabaya ni yapi? Vipi wanazifuata zile amrj 10 za mussa au nao wanazo za kwao?

10. Kosa la uzinzi kwa imani ya rastafarian lina tasfiri gani na adhabu zake ni zipi huku Duniani kwa imani yao.

NB: Waislam ukizini ni kupigwa mawe ufe, wakristo ni utalipwa mbinguni.

Nawasilisha[emoji4][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu,

Ningependa kuelimishwa haya machache kuhusiana na hii imani/dini ya Rastafarian (nikipata na ya ziada ntashukuru Mungu)...
A: YESU si Mtume bali ni MUNGU (Cheo katika Utatu Mtakatifu)
MFANO: Yai (Ganda + Nyama nyeupe + Kiini)
MWANZO 1:26. (UUMBAJI WA ULIMWENGU)
ISAYA 9:6.
YOHANA 1:1-5, 14.
1 YOHANA 5:20.
YOHANA 14. (KAZI KATIKA UMOJA WA YEHOVA + YESU + ROHO MTAKATIFU).

B: Adhabu ya uzinzi kwa Wakristo si mpaka mbinguni bali huanzia hapa hapa duniani kwa kukosa baraka za;
✓ Kiroho
✓ Kiafya.
✓ Kimwili
✓ Kiuchumi
✓ Kiakili.

1 WAKORINTHO 6:12-20.

MFANO WA ATHARI ZA UZINZI:

* Nabii Daudi aliadhibiwa vikali kwa kuzini na Mke wa Mtu (Bethsheba) wa Askari wake Daudi baada ya kumpeleka vitani auwawe ili ajiopolee mzigo.

Alipozini na Bethsheba na kuzaa naye Mtoto ilimchukiza MUNGU akaahidi kumuua mtoto wa Daudi, mbali na Daudi kufunga usiku na mchana kwa siku 7 zote akiomba rehema na neema za Mungu asipatwe na adhabu ya kifo cha Mtoto wake lakini bado Mtoto alikufa.

* Abisalom Mtoto wa Daudi alizini na Dada yake wa tumbo moja na Masuria wa Baba yake Mzazi Daudi.

* Abisalom Mtoto wa Daudi alihaini utawala wa ufalme wa Baba yake Mzazi kwa kumpindua na Daudi alikimbilia mafichoni ili kujiepusha na kifo toka kwa Mwanaye Abisalom.
 
Habari wakuu,

Ningependa kuelimishwa haya machache kuhusiana na hii imani/dini ya Rastafarian (nikipata na ya ziada ntashukuru Mungu)...
Nakujibu kwa uchache Yale ninayoyajuwa, kimsingi Rastafarian wana maingiliano na Ukristo ila shida IPO kwenye mapokeo tu.

Rastafarian wanaamini Biblia ila wengi ni waumini wa kanisa la Greek Orthodox.

Kwa jinsi nilivyokaa karibu na hawa watu kipindi Fulani kwa imani yao wanaamini Haile Selasie ndio Yesu Masiah, yani Wakristo wanasubili Yesu atarudi tena duniani kuwahukumu wazima na watu, lakini Rastafarian wanaclaim Haile Selassie ndio Yesu.

Kuhusu bangi hiyo kwao ni sacrament lakini siyo lazima kuvuta, kuwa Rastafarian pia siyo lazima ufuge Rasta.

Rastafarian wao wanaamini asili yao ni Wakushi yani Waethiopia, kwahiyo Ethiopia kwao ndio nchi yao takatifu.

Kuhusu nyama Rastafarian wao ni vegetarian, nadhani ukielewa maana ya vegetarian huwezi kuuliza swali zaidi, tena wengine hata mayai hawali wanaamini Yana uhai.

Katika dini zote ninazozijuwa ukikutana na Rastafarian wa kweli hawa ndio watu wanaongoza kwa roho nzuri, kauli mbiu yao peace and love.

Nimekudadavulia machache wajuzi watakutosheleza.
 
DeepPond yaani mama j kakupiga matukio mpaka unataka kuwa rasta? Kweli wanawake ni kiumbe dhaifu lakini anaweza kukutoa kabisa kwenye ramani
Ha ha ha....Hata hamna mkuu

Nmevutiwa Sana kuijua iman Yao iko vp,

Mana Nmegundua
mbali na kuvuta kwao bangi
Hawa jamaa Ni hawaibi,hawadhurumu, wakarimu,waaminifu na watu POA Sana kuishi nao mtaani[emoji4]
 
Rastafarian ikimaanisha wafuasi wa Ras Tafar (Haile Selassie).

Kwa uelewa wangu hafifu ni imani ambayo imejikita kwenye uafrika zaidi ingawa wanafuata biblia.

Haile Selassie kutoka Ethiopia (wakiumuita mfalme wa wafalme, bwana wa mabwana na simba mshindi wa kabila la yuda) ndo Messiah wao.

Hawatumii nyama na wanasisitiza amani na upendo, kama alivyosema mkuu hapo juu ni watu wakarimu sana.
 
Kitu ambacho nilikuwa sikifahamu kwamba nao wanatumia Biblia kama kitabu Chao Cha dini. Kuna Wakati niliwahi sikia mahojiano Yao Redioni, jamaa alidai wanavitabu vingine vya maarifa ila ni Moja kati ya vitabu vilivyofichwa. Na kuvipata ni shida maana ni kama kuza bangi.

Ila Nina njaa ya kuijua Imani hii.
 
Habari wakuu,

Ningependa kuelimishwa haya machache kuhusiana na hii imani/dini ya Rastafarian (nikipata kujuzwa na ya ziada ntashukuru sana).

1. Naskia rastafarian hawanywi pombe hivi Ni kweli? Kama ni kweli je, ni kwanini?

2. Nasikia hawali kitimoto je, kweli? Kwanini?

3. Nasikia ni marufuku kuhudhuria au kulia msibani je, ni kweli? Kama ni kweli kwanini? Wao rastafarian wakifariki nini kinafanyika? Hawazikwi au inakuaje?

4. Naskia kuvuta bangi kwao ni sehemu ya ibada je ni kweli? Kama ni kweli kwanini? Hivi ni lazima ukiwa rastafarian uvute bangi?

5. Hawa rastafarian mtume wao ni nani Kama ilivo kwa Islamic (Mohammad) Chirstian (Yesu).

6. Hawa rastafarian wanacho kitabu kitakatifu Kama ilivo kwa christians (Biblia) na Islamic (Quran)

7. Nasikia kwa rastafarian ni marufuku kula nyama nyekundu wala mayai ni kweli? Kama ni kweli kwanini?

8. Hawa rastafarian wanazungumziaje habar za kufa, kifo na habari kufuliwa upya uko mbinguni?

9. Hawa rastafarian wanazungumziaje kuhusu wale wanaotenda yale mema & mabaya hapa Duniani, malipo yao itakuaje uko mbinguni. Yaani kwao imani yao mema ni yapi na mabaya ni yapi? Vipi wanazifuata zile amrj 10 za mussa au nao wanazo za kwao?

10. Kosa la uzinzi kwa imani ya rastafarian lina tasfiri gani na adhabu zake ni zipi huku Duniani kwa imani yao.

NB: Waislam ukizini ni kupigwa mawe ufe, wakristo ni utalipwa mbinguni.

Nawasilisha[emoji4][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kijana yuko kijiweni wanapiga story kaona aanzishe Uzi kupata majibu
 
mimi mwenyewe ni mtu wa namna hiyo,kwanza kabisa unapozungumzia iman ya rastafari ni kweli ipo ila ni ya uzushi kwa sehemu kubwa,isipokuwa ww mwenyewe unaweza kuzaliwa na imani hiyo pasipokuwa hata na dred rocks,ila pia unapaswa kujua unapopewa sifa ya ras,tambua kabisa wewe ni mtu maalumu na ni tofauti na wenzio pia unakuwa katika mfumo wa maisha tofauti kabisa na binadamu wenzio hususani kwanzia kimwili,akil,roho mpaka utu,mengine nitaendeleza
 
Rastafari sio imani au dini ni way of life pure and clean as given by the most High(njia ya maisha masafi kama atakavyo Mungu).

Haile Sellasie I (Ras Tafari), Ras ni jina au cheo kinachomaanisha Head kama vile head of state, ni cheo cha juu alichokuwa anapewa kiongozi au mtawala anayeongoza nchi kwa misingi ya kiroho yaani mfalme wa amani.
Japo Rastafari inahusishwa na uafrika zaidi kwa kuwa ndio chimbuko lake, ila dhana yao imejikita kwenye kuishi maisha masafi kiroho kama vile ukarimu, upendo, amani, kutodhulumu au kuiba pia na usafi wa roho kwa njia ya chakula kwa kutokula nyama au kiumbe chochote kinachojongea, wao hula matunda na mboga za majani yaani vyakula vinavyochipuka ardhini. Hawali nyama wanaamini nyama ni najisi itaunajisi mwili katika hili kuna baadhi ya makundi ya kiroho pia wanaunga mkono kama vile budhist, taoist na hinduism.

Hawanywi pombe kwa kuwa wanaamini pombe ni haramu inanajisi na kuharibu mwili.

Bangi sio lazima kutumia ila wanaruhusu na pia inatumika hata katika vipengele vya ibada kama meditation, hawaichukulii kama starehe kama wafanyavyo masela wa uswahilini, kwao bangi ni mmea takatifu.

Siku yao ya ibada ni siku ya saba ya juma ama Sabato, kitabu chao ni biblia ila versio ya ki Orthodox, pia kuna kitabu wanachokiamini ambacho hakipatikani bookstore yeyote kinapatikana Ethiopia pekee ambapo kimefichwa mapangoni haruhusiwi mtu kusoma ila ni yule tu aliyefikisha level ya Monk wa kiorthodox, inaaminika ndiyo biblia kongwe kuliko zote duniani na ina vitabu vingi kuliko biblia hizi toleo jipya.

Sio lazima ufuge dread ndo uwe rasta lakini pia sio kila mwenye dread ni rasta.

Uzinzi kwao mwiko wanaamini inapunguza nguvu za kiroho na kushindwa kuconnect High Powers za Most High au Mungu, hivyo hutumika kama njia ya creation or meditative sex yaani sacred sex.

Kwao Haile Selasie wanamchukulia kama Mesiah kwa sababu ndio the last standing African strong emperor, aliyekuwa na upendo kwa watu weusi.
Kuhusu kumuabudu kama Mungu wa wanaamini binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu hivyo ni jitihada zako za kuishi maisha safi na matakatifu ndizo zitakusaidia kuuhuisha uungu uliopo ndani yako hivyo ukifika hizo level we ni Mesiah pia.

Kuhusu kifo wanaamini rasta never die, kinachokufa ni mwili ila roho itaishi milele.

Bado natafuta maarifa zaidi kwa sasa ni hayo niyajuayo ila pia ni rasta mtarajiwa nitapofanikiwa kuyashinda ya dunia yanayonikwamisha katika njia hii ya maisha ya uzima.

I n I, peace and love.
 
Habari wakuu,

Ningependa kuelimishwa haya machache kuhusiana na hii imani/dini ya Rastafarian (nikipata kujuzwa na ya ziada ntashukuru sana).

1. Naskia rastafarian hawanywi pombe hivi Ni kweli? Kama ni kweli je, ni kwanini?

2. Nasikia hawali kitimoto je, kweli? Kwanini?

3. Nasikia ni marufuku kuhudhuria au kulia msibani je, ni kweli? Kama ni kweli kwanini? Wao rastafarian wakifariki nini kinafanyika? Hawazikwi au inakuaje?

4. Naskia kuvuta bangi kwao ni sehemu ya ibada je ni kweli? Kama ni kweli kwanini? Hivi ni lazima ukiwa rastafarian uvute bangi?

5. Hawa rastafarian mtume wao ni nani Kama ilivo kwa Islamic (Mohammad) Chirstian (Yesu).

6. Hawa rastafarian wanacho kitabu kitakatifu Kama ilivo kwa christians (Biblia) na Islamic (Quran)

7. Nasikia kwa rastafarian ni marufuku kula nyama nyekundu wala mayai ni kweli? Kama ni kweli kwanini?

8. Hawa rastafarian wanazungumziaje habar za kufa, kifo na habari kufuliwa upya uko mbinguni?

9. Hawa rastafarian wanazungumziaje kuhusu wale wanaotenda yale mema & mabaya hapa Duniani, malipo yao itakuaje uko mbinguni. Yaani kwao imani yao mema ni yapi na mabaya ni yapi? Vipi wanazifuata zile amrj 10 za mussa au nao wanazo za kwao?

10. Kosa la uzinzi kwa imani ya rastafarian lina tasfiri gani na adhabu zake ni zipi huku Duniani kwa imani yao.

NB: Waislam ukizini ni kupigwa mawe ufe, wakristo ni utalipwa mbinguni.

Nawasilisha[emoji4][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
Rasta ni mtu anayemwabudu haile sellasie ( the lion of judah)na ni mfuasi wa Marcus Gravey, rasta ni peace& love , sio kila anayefuga dread ni rasta japo dread ni tamaduni za marasta, na bangi ni mmea wa uzima kwa rasta, rasta hawapendi utumwa ndo maana utaona rasta wengi wamejiajili aswa kwenye sanaa na music, pombe ni drugs kwa rasta ,
 
Kwa hiyo hawamwabudu Mungu?
 
Habari wakuu,

Ningependa kuelimishwa haya machache kuhusiana na hii imani/dini ya Rastafarian (nikipata kujuzwa na ya ziada ntashukuru sana).

1. Naskia rastafarian hawanywi pombe hivi Ni kweli? Kama ni kweli je, ni kwanini?

2. Nasikia hawali kitimoto je, kweli? Kwanini?

3. Nasikia ni marufuku kuhudhuria au kulia msibani je, ni kweli? Kama ni kweli kwanini? Wao rastafarian wakifariki nini kinafanyika? Hawazikwi au inakuaje?

4. Naskia kuvuta bangi kwao ni sehemu ya ibada je ni kweli? Kama ni kweli kwanini? Hivi ni lazima ukiwa rastafarian uvute bangi?

5. Hawa rastafarian mtume wao ni nani Kama ilivo kwa Islamic (Mohammad) Chirstian (Yesu).

6. Hawa rastafarian wanacho kitabu kitakatifu Kama ilivo kwa christians (Biblia) na Islamic (Quran)

7. Nasikia kwa rastafarian ni marufuku kula nyama nyekundu wala mayai ni kweli? Kama ni kweli kwanini?

8. Hawa rastafarian wanazungumziaje habar za kufa, kifo na habari kufuliwa upya uko mbinguni?

9. Hawa rastafarian wanazungumziaje kuhusu wale wanaotenda yale mema & mabaya hapa Duniani, malipo yao itakuaje uko mbinguni. Yaani kwao imani yao mema ni yapi na mabaya ni yapi? Vipi wanazifuata zile amrj 10 za mussa au nao wanazo za kwao?

10. Kosa la uzinzi kwa imani ya rastafarian lina tasfiri gani na adhabu zake ni zipi huku Duniani kwa imani yao.

NB: Waislam ukizini ni kupigwa mawe ufe, wakristo ni utalipwa mbinguni.

Nawasilisha[emoji4][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
Post in thread 'Philosophy of Religion: Uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa hoja ya Ufunuo na maandiko matakatifu' Philosophy of Religion: Uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa hoja ya Ufunuo na maandiko matakatifu
 
Nakujibu kwa uchache Yale ninayoyajuwa, kimsingi Rastafarian wana maingiliano na Ukristo ila shida IPO kwenye mapokeo tu.

Rastafarian wanaamini Biblia ila wengi ni waumini wa kanisa la Greek Orthodox.

Kwa jinsi nilivyokaa karibu na hawa watu kipindi Fulani kwa imani yao wanaamini Haile Selasie ndio Yesu Masiah, yani Wakristo wanasubili Yesu atarudi tena duniani kuwahukumu wazima na watu, lakini Rastafarian wanaclaim Haile Selassie ndio Yesu.

Kuhusu bangi hiyo kwao ni sacrament lakini siyo lazima kuvuta, kuwa Rastafarian pia siyo lazima ufuge Rasta.

Rastafarian wao wanaamini asili yao ni Wakushi yani Waethiopia, kwahiyo Ethiopia kwao ndio nchi yao takatifu.

Kuhusu nyama Rastafarian wao ni vegetarian, nadhani ukielewa maana ya vegetarian huwezi kuuliza swali zaidi, tena wengine hata mayai hawali wanaamini Yana uhai.

Katika dini zote ninazozijuwa ukikutana na Rastafarian wa kweli hawa ndio watu wanaongoza kwa roho nzuri, kauli mbiu yao peace and love.

Nimekudadavulia machache wajuzi watakutosheleza.
You dont haffi dread to be rasta,this is not a dread thing divine confession of the heart-Morgan heritage! Itafute hiyo ngoma utaelewa!
I n I rasta!! Nyabinghi!
Reggae music again-busy signal
Hey rastaman-Lucky dube
 
Back
Top Bottom