yamalenko
New Member
- Jun 22, 2021
- 4
- 7
Well said Rasta,imani safi kuweza kuishuhudia katika huu ulimwengu. sema inapigwa vita sana na mabepari. kwa kuwa ipo sana kinyume na matakwa yao. Rastafari imejikita katka kumkomboa binadamu asiwe mtumwa wa fikra.kwa hiyo kuna uongo mwingi sana wanazushiwa Rasta waonekane ni watu wa ajabu. Usipokuwa mfuatiliaji na mdadisi unarishwa tango pori. Jah Rastafaray Haille Sellasie HighRastafari sio imani au dini ni way of life pure and clean as given by the most High(njia ya maisha masafi kama atakavyo Mungu).
Haile Sellasie I (Ras Tafari), Ras ni jina au cheo kinachomaanisha Head kama vile head of state, ni cheo cha juu alichokuwa anapewa kiongozi au mtawala anayeongoza nchi kwa misingi ya kiroho yaani mfalme wa amani.
Japo Rastafari inahusishwa na uafrika zaidi kwa kuwa ndio chimbuko lake, ila dhana yao imejikita kwenye kuishi maisha masafi kiroho kama vile ukarimu, upendo, amani, kutodhulumu au kuiba pia na usafi wa roho kwa njia ya chakula kwa kutokula nyama au kiumbe chochote kinachojongea, wao hula matunda na mboga za majani yaani vyakula vinavyochipuka ardhini. Hawali nyama wanaamini nyama ni najisi itaunajisi mwili katika hili kuna baadhi ya makundi ya kiroho pia wanaunga mkono kama vile budhist, taoist na hinduism.
Hawanywi pombe kwa kuwa wanaamini pombe ni haramu inanajisi na kuharibu mwili.
Bangi sio lazima kutumia ila wanaruhusu na pia inatumika hata katika vipengele vya ibada kama meditation, hawaichukulii kama starehe kama wafanyavyo masela wa uswahilini, kwao bangi ni mmea takatifu.
Siku yao ya ibada ni siku ya saba ya juma ama Sabato, kitabu chao ni biblia ila versio ya ki Orthodox, pia kuna kitabu wanachokiamini ambacho hakipatikani bookstore yeyote kinapatikana Ethiopia pekee ambapo kimefichwa mapangoni haruhusiwi mtu kusoma ila ni yule tu aliyefikisha level ya Monk wa kiorthodox, inaaminika ndiyo biblia kongwe kuliko zote duniani na ina vitabu vingi kuliko biblia hizi toleo jipya.
Sio lazima ufuge dread ndo uwe rasta lakini pia sio kila mwenye dread ni rasta.
Uzinzi kwao mwiko wanaamini inapunguza nguvu za kiroho na kushindwa kuconnect High Powers za Most High au Mungu, hivyo hutumika kama njia ya creation or meditative sex yaani sacred sex.
Kwao Haile Selasie wanamchukulia kama Mesiah kwa sababu ndio the last standing African strong emperor, aliyekuwa na upendo kwa watu weusi.
Kuhusu kumuabudu kama Mungu wa wanaamini binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu hivyo ni jitihada zako za kuishi maisha safi na matakatifu ndizo zitakusaidia kuuhuisha uungu uliopo ndani yako hivyo ukifika hizo level we ni Mesiah pia.
Kuhusu kifo wanaamini rasta never die, kinachokufa ni mwili ila roho itaishi milele.
Bado natafuta maarifa zaidi kwa sasa ni hayo niyajuayo ila pia ni rasta mtarajiwa nitapofanikiwa kuyashinda ya dunia yanayonikwamisha katika njia hii ya maisha ya uzima.
I n I, peace and love.